Showing posts with label 2017 at 05:51PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 05:51PM. Show all posts
Bajeti 2017/18 inaenda kuwagusa wengi -Dkt Kigwangalla

Bajeti 2017/18 inaenda kuwagusa wengi -Dkt Kigwangalla

Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na watoto, Dkt Hamisi Kigwangalla amesema katika miaka yake 7 ya uwakilishi bungeni hajawahi kushuhudia bajeti ikishangiliwa kama ya Wizara ya Fedha huku akisema bajeti hiyo inaenda kuwagusa watu wengi.
Dkt Kigwangalla ametumia ukurasa wake wa Instagram kuisifia bajeti hiyo.
Katika miaka yangu saba ya uwakilishi #Bungeni sijawahi kushuhudia bajeti ikishangiliwa na wabunge kama ya jana. Kwa hakika bajeti ya 2017/18 inaenda kuwagusa watu wengi, kuanzia wakulima wetu wadogo wadogo hadi wakubwa hadi wenye viwanda vyenye fungamanisho na kilimo; wachimbaji wadogo hadi wakubwa. Kila mtu ameguswa. Dr. Mpango amekuja akiwa amejipanga haswa, kwa niaba ya Serikali yetu nzima. Michango mingi ya Wabunge na Mawaziri ameizingatia sana. Naamini huu usikivu ndiyo sababu ya bajeti kupendwa na kushangiliwa kiasi hicho. Kwa hakika itapita bila shida. Tutabaki na kazi ya kufanya kazi kwa bidii kuitekeleza. #bajeti #Bajeti2017 #HK #HamisiKigwangalla #Dr_Kigwangalla #SiasaNiVitendo
Juzi Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango aliwasilisha bungeni mapendekezo ya makadirio ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2017/18.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rZZJAU
via IFTTT


Afisa wa trafiki ashtumiwa kwa kuwakata nywele wanawake Nigeria

Afisa wa trafiki ashtumiwa kwa kuwakata nywele wanawake Nigeria

Mshauri wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, amelaani tendo hilo, ambalo amelitaja kuwa “udunishaji wa wanawake”
Kamanda mkuu wa usalama barabarani Nigeria awakata nywele wafanyikazi wa kike
Shirika la kudhibiti usalama barabarani nchini Nigeria, limemuadhibu kamanda wake mmoja mkuu, baada ya kupigwa picha ya video akiwaadhibu wafanyikazi wa kike kwa kuwakata nywele zao ndefu.
Picha zinazoonyesha kamanda huyo wa kiume, akichukua mkasi na kuanza kuwakata wafanyikazi wa kike waliokuwa kwenye foleni ya kukaguliwa, iliwekwa mtandaoni, na sasa imesabisha malumbano makubwa sio tu nchini Nigeria bali kote Afrika na Duniani.
Kuna sheria inayodhibiti mtindo wa nywele kwa wafanyikazi wa kike kwenye kampuni ya kitaifa ya usalama barabarani- Federal Road Safety Corp (FRSC).
Lakini msemaji amesema kuwa hatua ya kamanda huyo iko “nje ya” utendakazi wa FRSC.
Kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Lauretta Onochie, mshauri wa Rais wa Nigeria
Muhammadu Buhari, amelaani tendo hilo, ambalo amelitaja kuwa “udunishaji wa wanawake”.
Andrew Kumapayi, kamanda mkuu wa kikanda wa FRSC katika jimbo la Rivers State, anasemekana alitekeleza adhabu mapema asubuhi wakati wa gwaride katika mji wa Port Harcourt siku ya Jumatatu.
Hajatoa maelezo yoyote.
Kiongozi mmoja wa wafanyikazi wa kike wa shirika hilo (FRSC), anasema kuwa wanafaa
“kudumisha mtindo wa nywele ambao wanafaa kuingiza kwenye kofia zao za beret”, lakini hakutaja marufuku ya kuwa na nywele ndefu.
Ameitwa katika makao makuu ili kuzomewa baada ya picha hizo kusambazwa mtandaoni
Picha kwenye mtandao wa Facebook kuhusiana na tendo hilo kwa sasa zimefutwa kutoka kwa mtandao rasmi wa shirika hilo, ingawa picha hizo zimesambazwa mara elfu katika mitandao ya kijamii.
Maandishi katika mtandao huo ulisema kuwa Bw Kumapayi, alikuwa akitekeleza ukaguzi wa “nywele, sare rasmi na makucha” kwa wafanyikazi.
Maafisa wengine waliohusika katika kisa hicho pia wameitwa katika makao makuu. Msemaji wa FRSC Bisi Kazeem, ameiambia shirika la habari la serikali ya Nigeria- NAN.
Uchunguzi unaendelea na “hatua kali itachukuliwa dhidi ya wote waliohusika” aliongeza.

from Blogger http://ift.tt/2oyUEzF
via IFTTT


Kategori

Kategori