Showing posts with label 2017 at 11:12AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:12AM. Show all posts
ITAZAME VIDEO ILIYOMPONZA LOWASSA HADI KUITWA POLISI

ITAZAME VIDEO ILIYOMPONZA LOWASSA HADI KUITWA POLISI

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa jana alipata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumanne, saa 4 asubuhi kwa ajili ya mahojiano.
Lowassa ambaye pia amewahi kuwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, hakupewa maelezo wala ufafanuzi wowote kuwa mahojiano hayo yatahusu nini hasa.
Licha ya kutoelezwa dhumuni la wito wote, kumekuwapo na tetesi ambazo hata yeye amekiri kuwa, huenda wito huo umetokana na kauli aliyoitoa mwishoni mwa juma kuhusu Masheikh wa Uamisho ambao wanashikiliwa na serikali kwa miaka minne sasa.
Akiwa katika futari hiyo aliyoalikwa, Lowassa alisema kuwa alipokuwa akigombea urais mwaka 2015, aliahidi kwamba, kama angeshinda, siku hiyo hiyo angewaachia viongozi hao wadini wanaoshikiliwa. Lakini kwa vile hakushinda, alimsihi Rais Magufuli kuingilia kati suala hilo la viongozi wanaoshikiliwa kwa miaka yote hiyo bila kesi.
Mbali na hilo, Lowassa aliwataka waislamu kutokuwa wa baridi sana, badala yake watafute lugha nyingine ya kuzungumza ambayo serikali itasikia ili kuachia viongozi wao wanaoshikiliwa. Jambo hili huenda ndilo lililopelekea Lowassa kuitwa, kwani lina sura ya uchochezi ndani yake.

//platform.twitter.com/widgets.js

Masheikh wa Uamisho wanaoshikiliwa nchini walikamatwa Zanzibar ambapo wanatuhumiwa kwa ugaidi.

from Blogger http://ift.tt/2sLSWN2
via IFTTT


Majambazi wajeruhi na kupora fedha na dhahabu katika mgodi

Majambazi wajeruhi na kupora fedha na dhahabu katika mgodi

Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia mgodi wa dhahabu wa wachimbaji wadogo katika kijiji cha Nyakavangala kilichopo katika tarafa ya Isimani wilayani Iringa na kupora fedha tasilimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 80 na gramu 400 za dhahabu huku wakiwajeruhi watu tisa.
Majeruhi wa tukio hilo la uporaji ambao baadhi yao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa wamesimulia tukio hilo lililotokea siku ya tarehe 9 mwezi huu majira ya saa moja jioni ambapo kundi hilo la watu walivamia mgodini hapo na kuanza kuwasaka watu waliowataja kwa majina na kuwalazimisha baadhi ya wachimbaji kuwaonesha walipo watu hao.
Baadhi ya majeruhi hao wameiomba serikali kujenga kituo cha polisi katika eneo hilo la mgodi ili kuimarisha usalama wakisema kuwa uporaji huo ulifanyika kwa muda mrefu huku kukiwa hakuna msaada wowote kutokana na eneo hilo kutokuwa na kituo cha polisi wala huduma ya mtandao wa simu hali iliyowafanya majambazi hao kufanya tukio hilo kwa muda wa zaidi ya saa kwakuwa walijua hawatabughudhiwa wala kufurushwa na vyombo vya usalama.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka waporaji hao tangu walipopata taarifa hizo hapo jana na kuongeza kuwa serikali inashirikiana na wachimbaji katika eneo hilo la Nyakavangala kuratibu ujenzi wa kituo cha polisi ili kudhibiti usalama wa eneo hilo huku muhudumu wa afya wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa Bi Gloria Mnyonge akielezea hali za majeruhi hao.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2reiXFI
via IFTTT


Matokeo ya michezo ya kufudhu kombe la dunia,Ronaldo kama kawa acheka na nyavu.

Matokeo ya michezo ya kufudhu kombe la dunia,Ronaldo kama kawa acheka na nyavu.

Timu ya taifa ya Ureno ilikuwa uwanja wa ugenini kuikabiri timu ya taifa ya Latvia ambapo Ureno waliibuka kidedea kwa mabao matatu kwa sifuri huku mabao ya Ureno yakiwekwa kimiani na Cristiano Ronaldo aliyefunga mara mbili na Andre Silva akifunga moja.
Mabao hayo ya Cristiano Ronaldo yamemfanya afikishe jumla ya mabao 73 ambapo anakuwa mchezaji wa 3 kuwahi kuifungia timu yake ya taifa mabao mengi zaidi katika bara la Ulaya, katika mchezo mwingine timu ya taifa ya Uholanzi imeshusha kipigo cha mbwa mwizi kwa Lexembourg cha mabao matano kwa sifuri.
Mabao ya Uholanzi yalifungwa na Arjen Robbben,Wesley Sneijder,Wijnaldum,Quincy Prommes na Vincent Jenssen waliofunga moja moja huku Belarus wakiifunga Bulgaria kwa mabao mawili kwa moja, Andorra wakaifunga Hungary bao moja kwa sifuri,
Ubelgiji kupitia kwa Mertenes na Nacer Chadli waliifunga Estonia mabao mawili kwa sifuri na Switzerland nao wakaifunga Faroe mabao mawili kwa nunge, Ugiriki na Bosnia wakatoka uwanjani bila kufungana huku Cyprus wakiifunga Gibraitar mabaop mawili kwa moja.
Timu ya taifa ya Sweden ilikuwa nyumbani kuikabili Ufaransa na wakafanikiwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuibwagiza Ufaransa mabao mawili kwa moja na mabao ya Sweden yakifungwa na Jimmy Durmaz na Ola Toivonen huku lile la Ufaransa likifungwa na Olivier Giroud.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t5seME
via IFTTT


Nape Nnauye Amvaa Tena Mkuu wa Mkoa Sakata la Kuvamia Clouds Media

Nape Nnauye Amvaa Tena Mkuu wa Mkoa Sakata la Kuvamia Clouds Media

IKIWA ni miezi miwili imepita tangu kutokea tukio la uvamizi wa kituo cha Clouds Media Group na kuundwa kwa kamati ya kuchunguza tukio hilo, hatimaye aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemvaa tena Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kusema kwamba hakuunda kamati ya kumchunguza yeye, bali aliunda kamati ya kuchunguza tukio la kuvamiwa kwa kituo cha utangazaji cha Clouds Media Group.
“Niliunda kamati kuchunguza tukio la kuvamiwa kituo cha utangazaji sio kumchunguza RC. Kama RC alikuwa mmoja wa wavamizi, hayuko juu ya sheria,” ameandika Nape kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Alipoulizwa kwanini Waziri wa Habari aunde kamati ya uchunguzi wa tukio la uvamizi badala ya kamati hiyo kuundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Nape alijibu kwa kuuliza swali kama kila kamati inaundwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Majibu haya ya Nape yamekuja ikiwa ni saa chache baada ya kuulizwa ni yapi maoni yake kuhusu kauli ya Makonda kwamba hakuwa akifahamu mipaka yake ya kazi ndio sababu alikwenda kuunda tume ya kumchunguza.
Kauli ya Nape kuhusu kuunda kamati imekuja ikiwa ni takribani saa 24 tangu Makonda aliposema kuwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo aliunda kamati ya kumchunguza.
Makonda alisema hayo jana, ambapo alidai kuwa kamati iliyoundwa na Waziri isingeweza kumhoji kwa sababu haikuwa na uwezo huo kutokana na wajumbe wa kamati hiyo kutofahamu mambo yanayohusiana na masuala ya uvamizi.

from Blogger http://ift.tt/2qOl9Sx
via IFTTT


KAMBI ya Upinzania Bungeni Yamlima Barua IGP Mangu..Ni Kuhusu Vurugu za Lipumba Cuf..!!!

KAMBI ya Upinzania Bungeni Yamlima Barua IGP Mangu..Ni Kuhusu Vurugu za Lipumba Cuf..!!!

KAMBI ya Upinzani bungeni imemwandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu na taasisi za Serikali kuhoji tukio la mkutano wa ndani wa Chama cha Wananchi (CUF) mkoa wa Dar es Salaam kuvamiwa na watu wenye silaha juzi.
Watu wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba walivamia mkutano wa mwenyekiti wa mkoa na wanahabari wakiwa na bastola, fimbo na mikanda na kutishia maisha, kupiga watu waliokuwa kwenye ukumbi wa hoteli moja jijini na kufanya virugu.
Aidha, upinzani umemtupia lawana Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kuhusu uvamizi huo kwa kuwa hawakutekeleza majukumu yao.
Kadhalika, umelaani kitendo hicho cha uvamizi wa mkutano pamoja na waandishi wa habari kupigwa kwa kuitaka Serikali kutoa tamko na kuchukua hatua kali dhidi ya waliohusika.
Mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni wa CUF, Ally Saleh akizungumza kwa niaba ya wenzake alisema makundi ya uvamizi yamekuwa tishio katika jamii.
“CUF kimeshamwandikia barua IGP na taasisi zinginezo za Serikali kuonyesha matatizo yaliyotokea jana (juzi) na chanzo cha matatizo hayo,” alisema Saleh. “Tunangojea Serikali itasema nini juu ya tukio lile.”
Saleh ambaye pia ni Naibu mnadhimu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) bungeni, alisema kitendo kilichotokea katika mkutano wa CUF cha watu kuvamia na kutoa bastola hadharani hakina utofauti na tukio alilofanyiwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
Alisema ukimya wa Waziri Mwigulu na Dk. Mwakyembe juu ya tukio hilo umeonyesha hawajatimiza majukumu yao; hususani Waziri Mwakyembe ambaye alipaswa kuhakikisha waandishi wa habari wanakuwa salama.
“Mambo haya yanavyotokea mawaziri wawili tunataka kuwavisha mnyororo Waziri Mwigulu Nchemba na Mwakyembe,” alisema.
“Mwakyembe alipaswa kujitokeza kwa haraka na kutoa tamko dhidi ya kitendo walichofanyiwa waandishi, tunahisi kwamba jukumu a Serikali halijatekelezwa, Mwakyembe anapaswa kuhakikisha usalama wa waandishi unakuwapo. Hivyo Mawaziri hawa wawili wanapaswa kutoa tamko.”
Alisema kikundi cha Mungiki siyo kigeni hapa nchini na Serikali inakifahamu lakini hakuna hatua zozote ambazo zimeshachukuliwa hadi sasa.
Kadhalika, alisema Kutokana na tukio lililotokea juzi, mkutano wa ndani wa kikatiba uliotakiwa kufanywa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad leo Serikali wameufuta kitendo ambacho siyo sahihi.
Alisema kitendo cha Serikali kuufuta mkutano huo siyo sawa kwa sababu Profesa Lipumba anabebwa na mbereko ya Serikali kwa kufanya mikutano ya ndani kila wakati.
Alisema Serikali inalea Jamhuri ndogo ndani ya Jamhuri, vile vile Serikali imekuwa inalea kambi ndogo ndani ya Buguruni na kwamba wanufaika zaidi wa mgogoro unaoendelea ndani ya CUF ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao dhumuni lao ni kuchukua majimbo yanayoongozwa na CUF katika uchaguzi mkuu ujao.

from Blogger http://ift.tt/2q5F5Ns
via IFTTT


Kuhusu Tamko la Mitandao ya Jamii Kufutwa..Ikulu Imetoa Tamko Hili..!!!

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Ikulu, Gerson Msigwa ameikanusha taarifa inayosambaa ikionyesha kuwa serikali inatishia kuifuta mitandao ya kijamii.
Taarifa hiyo iliyoonyesha imeandaliwa na Ikulu, ilieleza kuwa serikali haitasita kuifuta mitandao ya kijamii iwapo itabaini kuwa yote yanayoendelea hayana tija.
“Serikali inafuatilia kwa karibu yote yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii, na endapo itabaini haina tija,
Msigwa baadaye aliandika katika ukurasa wake wa Twitter akiwataka watanzania waipuuze taarifa hiyo kwa kuwa ni feki.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2nPll31
via IFTTT


Mwanafunzi wa darasa la 3 Yuko Hoi Baada ya Kuchapwa na Mwalimu

MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya St Joseph’s Girls mjini Busia anauguza majereha kwenye makalio na mbavu baada ya kuadhibiwa kinyama.
Amedai amefanyiwa unyama huo mwalimu wake.
Akielezea Swahilihub yaliyomkumba Jumatano, mwanafunzi huyo wa kike mwenye umri wa miaka minane ambaye jina lake tumelibana kutokana na sababu za kiusalama, alisema alilazwa juu ya meza kabla ya mwalimu kuamuru wanafunzi wanne wamshike miguu na mikono kisha akaanza kumcharaza viboko na kusababisha majereha.
Vilevile aliongeza mwanafunzi huyo kutoka mtaa wa Marachi alifichua kuwa sababu ya kupokezwa adhabu hiyo iliyofanyika Alhamisi wiki iliyopita ni baada ya kuwasilisha kazi ya ziada ya somo husika akiwa amechelewa.
“Mwalimu alitupa kazi ya ziada na wenzagu darasani wakawa wepesi kumaliza kazi hiyo. Tulikutana na mwalimu yuyo huyo akiwa zamu na aliponiuliza ‘unatoka wapi’ nikamweleza ‘natoka ofisini’ kupeleka kitabu cha kazi ya ziada. Papo hapo akaniambia nilale chini na kuamuru wanafunzi wanne wanishike kabla ya yeye kuanza kunichapa. Siku hiyo nilihisi uchungu kwa makalio na mbavu ingawa nilijikaza hadi nyumbani na kuwaeleza wazazi,” amesema mwanafunzi huyo.
Naye, mamake mwanafunzi huyo BI Racheal Wambui ameelezea masikitiko ya mwanawe kuumizwa baada ya daktari katika hospitali ya rufaa ya Busia kubaini kiwango cha majereha.
“Mtoto alifika nyumbani akichechemea na nikamuuliza ni kwa nini. Aliniambia mwalimu alimwadhibu hadi kumuumiza. Nilichukua hatua na kumpeleka hospitalini na daktari akabaini kuwa alikuwa ameumizwa vibaya mbavuni na makalio baada ya kupiga picha za X-ray,” amesema Bi Wambui.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Bi Florida Maliki amesema wamepokea habari kuhusu kisa hicho na wameanzisha uchunguzi kabla ya kuchukua hatua yoyote dhidi ya mwalimu huyo.
“Tumeanzisha uchunguzi kufuatia kisa hiki ili kutafuta ukweli kwa sababu tumepokea ripoti kinzani. Mtoto alisema alichapwa wakati wa mapumziko ya kwanza huku mwalimu naye akisema alikuwa katika darasa la nane wakati huo.”
Bi Maliki aliongeza, “Walimu hawaruhusiwi kuwaadhibu watoto kwa viboko ila sheria inaturuhusu tu kuwapa wosia. Kulingana na mwalimu wake wa darasa, mwanafunzi alikuwa darasani Alhamisi na Ijumaa kabla ya malalamishi kuwasilishwa Jumatatu juma hili.”
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI

from Blogger http://ift.tt/2nUlEGX
via IFTTT


Makonda Sasa Kupelekwa Mahakamani kwa Issue ya Vyeti Feki,Tundu Lissu Kuongoza Timu ya Mawakili ili Wamsulubu Kisheria..!!!

Makonda Sasa Kupelekwa Mahakamani kwa Issue ya Vyeti Feki,Tundu Lissu Kuongoza Timu ya Mawakili ili Wamsulubu Kisheria..!!!

Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amesema Jumanne wiki ijayo atafungua kesi ya jinai dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na madai ya kuwa na vyeti feki.
Jacob pia amesema, atamshtaki Makonda katika sekretarieti ya maadili ya utumishi wa umma, tume ya haki za binadamu pamoja na utawala bora.
Amesema kesi hiyo ambayo itaongozwa na mawakili Tundu Lissu pamoja na Peter Kibatara.
“Tunachosubiri ni wanasheria wamalize mchakato wa uchaguzi Chama cha Wanasheria Tanganyika (TSL) na mara watakaporejea kutoka Arusha tutakwenda mahakamani” amesema

from Blogger http://ift.tt/2mPiEvv
via IFTTT


Wivu wa Mapenzi Wasababisha Kifo cha Kichanga,Baba Yake Alikicharaza Bakora ya Kichwani..!!!

MKAZI wa Kijiji cha Chiwana wilayani humu, Said Kassim (20), ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumuua mtoto katika tukio la ugomvi na mkewe chanzo kikidaiwa ni wivu wa mapenzi.
Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, Zubery Mwombeji alisema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 9, mwaka huu saa 10 jioni.
Kamanda Mwombeji alisema tukio hilo lilitokea wakati mtuhumiwa huyo alikuwa akigombana Machi 9, mwaka huu na mzazi mwenzake, Mariam Mohamed Seleman akimtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.
Kamanda Mwombeji alifafanua kuwa katika tukio hilo, mtuhumiwa alimshambulia kwa kumpiga kwa fimbo ya mti wa muanzi akidai amechelewa kurudi kutoka shambani.
Alisema wakati ugomvi huo ukianza, mkewe alikuwa akitokea shambani huku akiwa amembeba mtoto wao, Amos Kassi mwenye umri wa(miezi mitatu).
Hata hivyo, alisema wakati wakiendelea na ugomvi huo, kwa bahati mbaya fimbo hiyo ilimpiga mtoto kichwani na kumsababishia maumivu makali.
Kamanda Mwombeji alisema baada ya tukio hilo, wazazi hao walimpeleka mtoto katika zahanati ya kijiji hicho kwa matibabu, lakini alifariki dunia saa 2:00 usiku siku hiyo hiyo.
Alisema mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamni kujibu shitaka linalomkabili.
Mganga aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu, Dk. Vitalis Lusasi, alisema mtoto huyo alipata mpasuko kisogoni na kusababisha damu kuvuja ndani kwa ndani.
WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUODOA TAKA KIZIMBANI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE

from Blogger http://ift.tt/2mrhbdW
via IFTTT


Kategori

Kategori