Showing posts with label 2017 at 02:01PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:01PM. Show all posts
FAMILIA ya Ndesamburo yakanusha kuwapo mgogoro wa rambirambi ya kati yao na CHADEMA

FAMILIA ya Ndesamburo yakanusha kuwapo mgogoro wa rambirambi ya kati yao na CHADEMA

Familia ya mbunge wa zamani wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo imeushtukia mchezo mchafu unaochezwa kuhusu rambirambi za kifo cha mwanasiasa huyo na kuwajia juu wanaozusha kuwapo kwa mgogoro kati ya familia hiyo na Chadema.
Mtoto wa marehemu, Lucy Owenya alisema jana kuwa uzushi huo unalenga kuichonganisha familia hiyo na viongozi wa kitaifa wa Chadema akiwamo Mwenyekiti Freeman Mbowe.
Katika baadhi ya mitandao ya kijamii, kuna taarifa zinazodai kuibuka kwa sintofahamu kati ya familia ya marehemu na viongozi wa Chadema akiwamo Mbowe na Katibu Mkuu wake, Dk Vincent Mashinji.
Taarifa hizo ambazo zimekanushwa vikali na familia, zinadai kiasi cha rambirambi kilichochangwa ndani na nje ya nchi ni zaidi ya Sh600 milioni, lakini familia imekabidhiwa Sh120 milioni tu.
Kwa mujibu wa madai hayo, fedha za rambirambi zinazodaiwa kuchangwa bila kupitia mikononi mwa familia ni zaidi ya Sh600 milioni, huku ikidaiwa Sh345 milioni zikichangwa kutoka Ujerumani.
“Sisi kama wanafamilia tunajiweka mbali na ujumbe huo wa kizushi wa namna hiyo wenye malengo mabaya ya kuichonganisha familia na mwenyekiti wetu Freeman Mbowe,” alisema Owenya. “Ukitazama ni kama wanataka kuibua hoja fulani kuwa kwa vile upande fulani kule Arusha ulituhumiwa kula fedha za rambirambi basi na huku tuwazushie viongozi wa Chadema.”
Ingawa hakufafanua, lakini rambirambi zilizoibua manung’uniko ni za wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent ya Jijini Arusha, ambao walipoteza maisha na zaidi ya Sh300 milioni zilichangwa.
Ndesamburo ambaye alikuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa vipindi vitatu mfululizo (2000-2015), alifariki dunia Mei 31, alipofikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Mwanasiasa huyo, alikuwa ofisini kwake Hoteli ya Keys, Moshi akitaka kusaini hati ya malipo, kwa ajili ya kukabidhi rambirambi kwa vifo vya wanafunzi wa Lucky Vincent.
Ilikuwa akabidhi Sh100,000 kwa kila familia iliyopatwa na msiba huo na ilikuwa akabidhi fedha hizo kwa Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ambaye alikuwa naye ofisini hapo. “Hata arobaini haijaisha wanaanza kuturudishia uchungu wa kumpoteza mzee kwa kueneza mambo ya uongo. Wamwache mzee (Ndesamburo) apumzike kwa amani. Wasitafute kick (sifa),” alisema Owenya.
Owenya ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), alikataa kutaja kiasi cha rambirambi kilichopatikana lakini akasisitiza kuwa wanaangalia njia bora za kisheria za kushughulikia suala hilo.
Akizungumzia suala hilo, Katibu wa Chadema Mkoa Kilimanjaro, Basil Lema alisema katika dhambi mbaya ambayo waliosambaza ujumbe huo wameipata, ni kuichonganisha Chadema na familia ya marehemu mzee Ndesamburo.
Lema, ambaye alikuwa Katibu wa Ndesamburo katika kipindi chote ambacho mzee huyo alikuwa mbunge, alisema taarifa za kutafunwa kwa rambirambi ni uongo na kulaani waliousambaza ujumbe huo.
Katibu huyo alisema Chadema makao makuu ndiyo iliyobeba kwa sehemu kubwa gharama za msiba huo na kwamba kila kiongozi wa Chadema aliyefika msibani alijigharamia.
Chanzo: Mwananchi
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rMBvZf
via IFTTT


Hivi Ndivyo Taifa Linavyoibiwa Madini Mchana Kweupee..!!!

Hivi Ndivyo Taifa Linavyoibiwa Madini Mchana Kweupee..!!!

Kamati iliyoundwa na Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kuchunguza mchanga wenye madini aliokuwa ameuzuia kusafirishwa nje ya nchi, hii ljana imewasilisha taarifa ya uchunguzi ilioufanya ikiwa na mambo 8 pamoja na mapendekezo 9.
Kamati hiyo imebaini mambo makuu 8 kama ifuatavyo……
1. Dhahabu
Kamati imebaini kuwepo kwa viwango vingi vya juu vya dhahabu ndani ya makinikia yaliyofanyiwa uchunguzi. Viwango hivyo ni kati ya 671 g/t hadi 2375 g/t, sawa na wastani wa 1400 g/t. Wastani huu ni sawa na 28 kg za dhababu kwenye kontena moja lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kwenye makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na wastani wa tani 7.8 za dhahabu yenye thamani ya TZS bilioni 676 (USD 307,292,720).
Aidha, kwa kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwenye kontena moja lenye shehena ya tani 20 za makinikia (47.5 kg), kiasi cha dhahabu katika makontena 277 kitakuwa 13,157.5 kg ambazo thamani yake ni TZS 1,146,860,330,000 (USD 521,300,150).
Hivyo, thamani ya dhahabu katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147.
Taarifa tulizopata kutoka kwa wazalishaji pamoja na Wakala wa Serikali wa Ukaguzi Madini (TMAA) zinaonesha kuwa makinikia yana wastani wa takriban 200 g/t. Kiwango hiki ni sawa na kilo 4 za dhababu kwenye kila kontena. Hivyo, makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu yatakuwa na tani 1.1 za dhahabu. Kiasi hiki cha dhahabu kina thamami ya TZS bilioni 97.5 (USD 44,320,000).
Thamani hii ni ndogo sana ukilinganisha na thamani halisi iliyopatikana katika uchunguzi huu ya kati ya TZS bilioni 676 na bilioni 1,147. Kutokana na tofauti hii kubwa kati ya viwango vya dhahabu vilivyopo kwenye taarifa za usafirishaji na vile ambavyo Kamati imevibaini, ni dhahiri kuwa Taifa linaibiwa sana kupitia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi.
2. Pamoja na viwango vikubwa vya dhahabu kwenye makinikia, Kamati ilipima na kupata viwango vikubwa vya madini ya copper (kiwango cha 15.09% hadi 33.78%, wastani wa 26%), silver (kiwango cha 202.7 g/t hadi 351 g/t, wastani wa 305 g/t), sulfur (kiwango cha 16.7% hadi 50.8%, wastani wa 39.0%) na iron (kiwango cha 13.6% hadi 30.6%,wastani wa 27%).
Copper
Wastani wa kiwango cha copper kilichopatikana ni tani 5.2 na kiwango cha juu kilichopimwa ni tani 6.75 kwenye kila kontena lenye tani 20 za makinikia. Hivyo, kiasi cha wastani wa copper kwenye makontena 277 ni tani 1,440.4 ambazo thamani yake ni TZS bilioni 17.9 (USD 8,138,260) na kiasi cha juu ni tani 1,871.4 ambazo zina thamani ya TZS bilioni 23.3 (USD 10,573,478). Hivyo, thamani ya copper katika makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini ni kati ya TZS bilioni 17.9 na bilioni 23.3.

from Blogger http://ift.tt/2rCNCM4
via IFTTT


FAMILIA NZIMA YASADIKIWA KULA SUMU KALI

FAMILIA NZIMA YASADIKIWA KULA SUMU KALI

“Watu saba wa familia moja katika kijiji cha Kibuhi wilaya ya Rorya mkoani Mara, wamefikishwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara mjini Musoma, kwa ajili ya matibabu, baada ya kula mboga za majani aina ya Mgagani zinazodaiwa kuwa na sumu na kusababisha kupatwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kupoteza fahamu huku baadhi yao wakirukwa na akili na hivyo kuwafanya kukimbia ovyo.

from Blogger http://ift.tt/2poYyZa
via IFTTT


AFANDE Sele Amrushia Dongo Kitila โ€ Kitila Ulikuwa Unaongea Sana Kabla Hujakaribishwa Mezaniโ€

AFANDE Sele Amrushia Dongo Kitila ” Kitila Ulikuwa Unaongea Sana Kabla Hujakaribishwa Mezani”

Kupitia ukurasa wa Facebook Afande Sele ameandika haya:
“Hongera Profesa Kitila Japo Kwa Shingo Upande Lkn Kupitia Wewe Nimejifunza Maana Ya Kuweka Akiba Ya Maneno Ili Elimu na Uungwana VIthibitishe Umuhimu Wake Ulimwenguni….Dah”Kitila Alikuwa Anaongee Saaana Kabla Hajakaribishwa Mezani…Sasa Na Yeye Yupo Mezani Kapewa Madikodiko Anakula….Mila Za Kikwetu Zinakataza Mtu Kuongea Wkt Wa KULA….Nasubiri Kuona Kama Kitila Atakiuka Mila Hiyo Kwa Kuendelea Kuongea Wkt Wa Kula Au Nae Atafuata Mkumbo Kwa Kukaa Kimya…..Dunia RangiRangile….” Afande Sele

from Blogger http://ift.tt/2oMepRU
via IFTTT


Rasmi..Diamond Avunja Ukimya Kuhusu Utajiri Wake..Aeleza A – Z Jinsi Anavyoupata..Wengi Wapigwa Butwaa..!!!

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’, amefichua moja ya siri ya mafanikio yake makubwa kiuchumi ni kusaidia watu wenye uhitaji.
Diamond ambaye anatajwa kama msanii anayeongoza kwa kipato nchini, amesema anajisikia ufahari mkubwa kuona anaweza kuwasaidia watu wenye uhitaji na amekuwa akipata baraka zaidi kupitia kazi zake.
“Unajua watu wengi hawajui ukitoa unazidi kubarikiwa, hii kwangu imekuwa sehemu ya mafanikio sana, huwa najisikia mwenye bahati kubwa nikimsaidia mtu mwenye uhitaji kwani naamini lazima nitafanikiwa,” alisema Diamond.
Alisema amekuwa akikutana na changamoto nyingi ikiwamo watu wengi kuhitaji msaada kutoka kwake, lakini amekuwa akiwalenga wale ambao yeye anaamini wanahitaji msaada zaidi kwake.
Tazama video Mtoto amvua kofia
 Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2mVnkmQ
via IFTTT


Kategori

Kategori