Showing posts with label 2017 at 10:44AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 10:44AM. Show all posts
EXCLUSIVE: Fahamu Mambo 8 kuhusu Train za umeme zinazoletwa Tanzania

EXCLUSIVE: Fahamu Mambo 8 kuhusu Train za umeme zinazoletwa Tanzania

Rais JPM April 12, 2017 alizindua ujenzi wa reli ya kisasa ‘standard gauge’ kutoka DSM hadi Mwanza ambayo itakamilika Oct 2019 jambo lililozua gumzo kwa baadhi ya Wananchi wakiwa na wasiwasi kuhusu train hizo kutokana na tatizo la umeme.
Ayo TV na millardayo.com zimekutana na Mhandisi wa Miundombinu ya Reli ambaye pia ni Mkuu wa Mradi huu Maizo Mgeni kutoka Kampuni inayojihusisha na ujenzi wa reli Tanzania RAHCO na kuelezeea mambo makubwa manane yanayohusiana na Standard Gauge.
Mambo manane hayo ni:
1:      Treni itakuwa inasimama kwenye vituo sita kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo      itasimama Pugu, Soga, ruvu, Stesheni ya Ngerengere na mwisho Treni itasimama Morogoro.
2:     Kutokana na Treni kutumia umeme Serikali imejipanga kutoa umeme wa uhakika kwa 100% na wananchi wasiwe na shaka yoyote kwani umeme wa Treni hujengewa nyaya zake maalum zinazotofautiana na nyaya za umeme wa kawaida.
3:     Treni hii itakuwa na uwezo wa kusafirisha wagonjwa mahututi kwani ni za kisasa na zina mwendo wa haraka ambapo itatumia saa moja na nusu kutoka Morogoro hadi Dar es Salaam.
4:     Umeme utatumia vyanzo vyenye nguvu kutoa umeme wa Treni kama vyanzo vya maji na makaa ya mawe.
5:     Kwa tathmini ya sasa nauli ya Treni hizi haitokuwa sawa na Treni za mita kwani ni Treni zinazotumia teknolojia kubwa na za kisasa, hivyo nauli itakuwa juu zaidi ya Treni za kawaida.
6:     Treni haitosimama kama umeme kutoka Tanesco ukikatika ghafla.
7:     Kiwango cha nauli kwa wanafunzi bado kinafanyiwa kazi.
8:    Kwa sasa watu binafsi hawataruhusiwa kuwa na Treni binafsi kwani Shirika la Reli ndilo litakuwa msimamizi mkuu.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sbOSDd
via IFTTT


Kisa cha Polisi kuwapiga Mabomu ya Machozi Walemavu Dar

Kisa cha Polisi kuwapiga Mabomu ya Machozi Walemavu Dar

POLISI jana walitumia mabovu ya machozi kutawanya watu wenye ulemavu waliokuwa wamekusanyika na kufunga barabara ya Sokoine jijini Dar es Salaam.
Mabomu hayo yalizua taharuki kwa watumiaji wa njia hiyo na kusababisha usumbufu kwao uliodumu takriban dakika kumi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni, aliliambia Nipashe jana kuwa polisi walilazimika kutumia mabomu kama njia ya kuwakamata watu hao.
Kamanda Hamduni alisema kutokana na kitendo hicho, polisi wanawashikilia watu 40 akiwamo mwanamke mmoja.
Alisema lengo la mkusanyiko huo ulikuwa kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuwasilisha malalamiko yao dhidi ya kukamatwa na askari polisi wa usalama barabarani.

“Ni kweli tunawashikilia watu 40 akiwamo mwanamke mmoja kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.

“Watu hawa walikuwa wanakwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kupeleka malalamiko yao kuhusu kitendo cha kukamatwa na askari wa usalama barabarani,” alisema.

Kamanda Hamduni alisema baada ya polisi kufika eneo hilo na kutoa amri mara tatu ya kuwataka kutawanyika, walemavu walikaidi ndiyo maana waliamua kutumia mabomu ya machozi.
Alisema nguvu hiyo ya kutumia mabomu ilikuwa na lengo la kurahisisha ukamataji wa watu hao waliokaidi amri ya polisi kutawanyika.

from Blogger http://ift.tt/2txRICH
via IFTTT


Kategori

Kategori