Showing posts with label 2017 at 01:33PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 01:33PM. Show all posts
Mimba ya Hamisa Mobeto utata mtupu!!!…….

Mimba ya Hamisa Mobeto utata mtupu!!!…….

WAKATI yakisemwa mengi juu ya ujauzito alionao ambao kwa sasa hauhitaji miwani ili kuuona, mwanamitindo matata Bongo, Hamisa Mobeto amepasua jipu juu ya mimba hiyo kufuatia kutajwa kwa msanii wa Bongo Fleva.
Kwa siku kadhaa sasa, kumekuwa na habari nyingi juu ya Hamisa kudaiwa kubeba ujauzito wa jamaa huyo ilihali akijua msanii huyo ana mpenzi wake ambaye amekuwa akikwaruzana naye mara kwa mara.
HAMISA AJIFICHA
Ilielezwa kwamba, kufuatia maneno mengi juu ya jambo hilo, Hamisa amekuwa akijifi cha kukwepa vyombo vya habari, lakini Wikienda limefanikiwa kumbana na kufunguka mazito.
KWELI MJAMZITO
Hamisa ambaye wengi wamekuwa hawana uhakika kama kweli ni mjamzito, mbali na kukiri kuwa kweli ni mjamzito wa mtoto wa pili baada ya yule wa awali wa kike aliyezaa na bosi maarufu wa redio jijini Dar, aliliambia Wikienda kuwa, yanasemwa mengi juu ya mimba yake hasa aliyempachika lakini yeye hajali kwani yupo tayari kupokea matusi ya jumla na rejareja.
Wikienda: Je, ni kweli mimba ni ya msanii wa Bongo Fleva kama inavyosemekana?
Hamisa: Siko tayari kusema ujauzito ni wa nani. Watu waelewe hivyohivyo wanavyoelewa.
Wikienda: Lakini kila mtu anajua ni wa msanii huyo, je, ni kweli?
Hamisa: Wanaomtaja baba wa ujauzito wangu hawanisumbui kabisa na wakae wakijua hivyo.
Wikienda: Lakini huoni kwamba ni tatizo kuzaa tena nje ya ndoa baada ya yule wa kwanza uliyezaa na bosi wa redio bila kufunga ndoa?
Hamisa: Hayo ni maisha yangu na kama nilivyosema, maneno ya watu hayanisumbui.
Hata hivyo, mazungumzo kati ya Wikienda na Hamisa yaliishia hapo kwa maelezo kwamba hataki tena kuulizwa jambo hilo kwani kila kitu kinajulikana.
MIMBA YA PILI?
Hii ni mimba ya pili ambayo Hamisa anadaiwa kupachikwa na msanii huyo baada ya ile ya awali aliyopachikwa mwaka jana kuchoropoka na kuwa gumzo kubwa baada ya mpenzi wa mwanaume huyo kuja juu na kuanzisha bifu ambalo halijawahi kuzimwa hadi leo.
STORI: IMELDA MTEMA NA MUSA MATEJA | IJUMAA WIKIENDA, DAR
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tFr5Nv
via IFTTT


VIDEO: QUICK ROCKA ADAIWA MILIONI 20 KWA KUIBA WIMBO

Mwanamuziki Khalid Mohamed maarufu kwa jina la sanaa T.I.D amewataka wasanii wenzake wawili kumlipa faini ya Tsh milioni 20 kwa kile alichosema kuwa wametumia haki zake pasipokuwa na idhini yake.
T.I.D amewatakata Quick Rocka na OMG kumlipa fedha hizo baada ya kutumia wimbo wake Watasema Sana bila ridhaa yake jambo ambalo ni kinyume na sheria.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, T.I.D ameweka sehemu ya video ya wimbo huo na kuandika, “Wat is this….?! Hivi ndio mnapata Magari yenu!? @quickrocka & @omgtanzania we need to TALK #Watasema.”
Msanii huyo amesema kuwa wamenakili wimbo wake huo ambao ulimpatia tuzo mbili kutoka nchini Kenya mwaka 2005 (Kisima Music Awards 2005) na hivyo kabla hajafanya kitu kibaya wamlipe fedha hizo.
“Naomba tukutane Central Police huwezi kutumia Haki zangu hivihivi Kabla sijafanya kitu kibaya nahitaji million 20 compensation… This song ni Awards mbili Za Kisima Music Awards 2005 inKenya u can’t just Steal it, Unalala Ndani Leo.”
Video ya wimbo huwa wa Quick Rocka na OMG umetoka leo na unaweza kutazama video hiyo hapa chini;
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t9qmqv
via IFTTT


Tamko Kali la Kubenea Kuhusu Kukamatwa Kwa Meya wa Ubungo Boniface

Tamko Kali la Kubenea Kuhusu Kukamatwa Kwa Meya wa Ubungo Boniface

TAARIFA KWA UMMA*
NIMEPOKEA kwa masikitiko makubwa taarifa kuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Yakoub amekamatwa na jeshi la polisi kwa amri ya “wanaodai wako madarakani.”
Kukamatwa kwake kunatokana na hatua yake ya kumpokea Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Pwani, waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.
Mhe. Sumaye alikuwa na ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za Manispaa za Dar es Salaam ambazo ziko chini ya vyama vinavyounda umoja wa UKAWA.
Napenda kuufahamisha umma kuwa amri; na au maelekezo yoyote yaliyotolewa iwe na polisi au mkuu wa mkoa ama wilaya juu ya kukamatwa kwa Meya ni batili na haikubariki.
Hivyo basi, ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunapigana kufa na kupona kutetea haki za wananchi waliotuchagua na kuhakikisha Meya wetu anakuwa huru kwa gharama yoyote ile.
Ninawaomba wanachama, viongozi na wananchi wa jimbo la Ubungo na Kanda ya Pwani kusimama nasi, pamoja na Meya wetu katika kipindi kigumu cha kudai demokrasia ya kweli ndani ya Nchi yetu.
Ninaahidi kuwa mstari wa mbele kutetea wananchi na kuhakikisha haki zao zinapatikana.
Ni jukumu letu sote kuhakikisha “udikteta ulioanza kuingia nchini taratibu,” unatokomezwa.
Taifa hili siyo mali ya CCM. Ni letu sote.
*Saed Kubenea*
Mbunge wa Ubungo, M/M- Kanda ya Pwani.
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sKR1sC
via IFTTT


Mwakyembe: Ntahakikisha Nawapata Waliomteka Roma ili Kukomesha Tabia Hii..!!!

Mwakyembe: Ntahakikisha Nawapata Waliomteka Roma ili Kukomesha Tabia Hii..!!!

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesikitishwa na vitendo walivyofanyiwa wasanii wa muziki Roma Mkatoliki na wenzake huku akisema hawezi kukubali kuona mambo kama hayo yakiwa yanaendelea kutokea.
Akizungumza na wanahabari jana Jijini Dar es Salaam, Waziri huyo amesema kilichotokea siyo hali ya kawaida kwa watanzania kamwe hawezi kukubaliana na jambo hilo huku akisisitiza kuwa atafuatilia kwa ukaribu sana ili aweze kupata majibu ya haraka kabla hajawasilisha bajeti ya wizara yake
“Hiki kilichotokea siyo hali ya kawaida kwa watanzania, hatuwezi kukubali kitu kama hiki kiendelee kutokea,nitalifuatilia kwa ukaribu sana, nitajitahidi nipate majibu kabla ya bajeti yangu Bungeni”. Alisema Dk. Mwakyembe
Hata hivyo Dkt. Mwakyembe amewataka wananchi waache tabia ya kuamini kila maneno yanayosemwa na watu ambao hawana ujuzi katika masuala ya uchunguzi, hivyo wanapaswa kuvipa muda vyombo vya dola viweze kufanya kazi zake kwa ufasaha.
“Nilishasema kuwa nimeagiza vyombo vya dola vifanye uchunguzi ili ajulikane aliyewafanyia hivi wakina Roma kama ni nani kama wa dola ntadili naye, tuache uchunguzi ufanyike, tuache kupiga ramli”. Alisisitiza Mwakyembe
Pia Waziri huyo mwenye dhamana na wasanii ametoa ujumbe kwa vyombo vyote vilivyopo chini ya Wizara yake kutofanya mahojiano yoyote yanayowahusu wasanii hao bila ya kuwepo taarifa kamili kutoka kwake.
Kwa upande mwingine Roma ambaye ambaye amesimulia tukio lilivyokuwa amesema kwa sasa hawezi kuongea mambo mengi kwa kuwa kila kitu amekwisharipoti polisi kila kitu, na kwamba kuna mambo akiyaweka hadharani atakuwa anaingilia upelelezi wa polisi.
Pia amesema hawezi kujua kama kweli tukio hilo lililowatokea linahusiana na muziki kwa kuwa ameweza kuhusishwa mpaka mfanyakazi wao wa ndani ambaye hana hata chembechembe za uimbaji.

from Blogger http://ift.tt/2p0yneU
via IFTTT


Kategori

Kategori