Showing posts with label 2017 at 01:46PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 01:46PM. Show all posts
Mwanamke Anayefuga Ndevu Kama Mwanaume Avunja Rekodi ya Dunia………

Mwanamke Anayefuga Ndevu Kama Mwanaume Avunja Rekodi ya Dunia………

KATIKA umri wa miaka 25 alionao, mrembo Harnaam Kaur anashikilia rekodi ya dunia ya kuwa mwanamke mwenye nywele mwilini. Hata hivyo, ameikubali hali hiyo na kuamua kufuga ndevu, jambo linalowashangaza wengi, ikionekana ni jambo geni kwa wanawake.
Amedhihakiwa shuleni, mtaani, kazini kwake na hata katika mitandao ya kijamii, lakini kamwe hakuthubutu kuzinyoa nywele zake, akiamini Mungu alikuwa na sababu za kumfanya awe na mwonekano huo.
Ndiyo maana, leo hii ukikutana naye, ni sura na maumbile yake ya kike ndiyo yatakayokutambulisha kuwa ni mwanamke, ingawa kidevu chake kimechakaa ndevu mithili ya mwanaume, huku mdomo wake ukiwa umezungukwa pia.
Kaur ana tatizo la homoni lifahamikalo kwa Kiingereza kama polycystic ovary syndrome, ambalo humfanya mwanamke kuwa na nywele nyingi zaidi usoni. Anasema awali, wakati anaanza kuota ndevu baada ya kupevuka akiwa na umri wa miaka 11, alipata wakati mgumu shuleni na hata mtaani, akidhihakiwa, jambo lililomkera mno.
Akiwa na umri wa miaka 15, anasema kero dhidi yake zilizidi na hata kufikiria kutaka kujiua, kwani hakuyafurahia tena maisha na hata alilazimika kuwa mtoro shuleni. “Ndiyo, nilitaka kujidhuhuru kwa sababu ya hizi ndevu.
Kuna siku nilinunua vidonge vingi na kutaka kuvimeza ili nife, ulikuwa uamuzi wangu wa mwisho… lakini kama miujiza, sijui kilitokea nini sikuendelea kuwaza kujiua,” anasema Kaur, mkazi wa Slough huko Berkshire, Kusini Mashariki mwa England.
Anasema, awali alijaribu kila njia kuzinyoa nywele zilizokuwa zikiota usoni kwake. Alijaribu pia kubadilisha rangi ya ngozi, kunyoa, kutumia mafuta ya kuondoa nywele mwilini, lakini bila mafanikio. Ikafikia hatua ya kunyoa ndevu kila siku.
Lakini nywele hizo ziliendelea kuwa nyeusi na ndefu zaidi. “Nilikuwa na marafiki waliokuwa karibu nami, walinifariji lakini pia familia ilinisaidia katika wakati mgumu niliokuwa nao,” anasema. Anaongeza kuwa, baadaye alianza kujikubali na kufurahia maisha, licha ya kwamba watu wengi waliendelea kumshangaa.
Wapo pia waliotishia kumuua endapo ataendelea kuziacha ndevu zake. Na katika kuthibitisha kuwa amejikubali, Machi mwaka jana, Kaur alikuwa mwanamke wa kwanza kushiriki maonesho ya Wiki ya Mitindo London akiwa na ndevu zake, Amekuwa akishiriki pia maonesho mengine katika nchi mbalimbali.
Kwake, anasema ni heshima kubwa kwake kutambuliwa na kuwekwa kwenye Kitabu cha Rekodi za Dunia cha Guinness. Na baada ya kuacha ualimu, amekuwa mwanaharakati akipambana kuelemisha wanawake na wasichana wengine wenye matatizo ya aina yake wajiamini, kwani hawana tofauti na binadamu wengine.
“Kuna niliokosana nao kwa sababu niliamua kuachia ndevu zangu. Lakini nashukuru nimepata nguvu na sasa nataka kuionesha dunia kwamba hili ni tatizo la kawaida, watu hawapaswi kunyanyasika. “Binafsi nimegundua nina nguvu, mimi ni mrembo na mtu asiyeogopa.
Tuzo ya Guinness imenipa nguvu na ujasiri zaidi. Sasa ninajipenda kama mwanamke, ninavutia, nina marafiki na ninapata mikataba ya kazi, kimsingi maisha yanaendelea,” anasisitiza kimwana huyo ambaye amekiri kutokuwa na mahusiano kimapenzi, ingawa anaamini wakati ukifika atampata mwandani wake.
Chanzo:Habarileo
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tyVcHP
via IFTTT


Mbunge wa Geita Joseph Musukuma Afunguka Jinsi Atakavyowavimbisha Matumbo Wakazi wa Dar es Salaam

Mbunge wa Geita Joseph Musukuma Afunguka Jinsi Atakavyowavimbisha Matumbo Wakazi wa Dar es Salaam

Mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku Musukuma amesema hawezi kumsifia hata kidogo Prof. Jumanne Maghembe, Waziri wa Maliasili na Utalii kwani yeye na watu wake wa Wizara wanafanya mambo ya ajabu hasa kwa watu wa Kanda ya Ziwa.
Musukuma anasema watu wa Wizara ya Maliasili wamekuwa wakiuza ng’ombe za watu jamii ya wasukuma na kuzipiga mnada kwa dili kwa lengo la kujinufaisha wenyewe, hivyo mbunge huyo amesema wasukuma wameamua kuwa wataziroga ng’ombe zote ili wanaokula ngo’mbe hizo Dar es Salaam wavimbe matumbo.
“Napata shida sana kujiuliza labda sisi watu wa kanda ya ziwa labda tulikuja kwa bahati mbaya Tanzania hii, mbona yanayofanyika Kanda ya Ziwa hayafanyiki Kanda ya Kaskazini wakati nao wana mapori, Waziri ametoa siku tatu tukamatiwe ng’ombe kwa kisingizio kwamba ni ng’ombe za Wanyarwanda wakati huo huo watumishi wake wanaowaingiza Wanyarwanda wanawaambia toeni ng’ombe, mnaenda kukamata ng’ombe za Wasukuma halafu unazipiga mnada na mnada wenyewe unavyopigwa ni wa dili” Alisisitiza Musukuma 
Mbunge huyo aliendelea kuelezea namna watu wa Wizara ya Maliasili wanavyofanya minada hiyo huku wakiwaumiza wafugaji
“Yaani ng’ombe 600 unaambiwa ulete milioni tatu halafu wanatoa watu wao wa Ubungo sasa hapo nikupongeze kwa sababu gani? Tunajua mipango inayoendelea kwenye wizara yako na niliwapigia kabisa watumishi wako, wananiambia mliipenda wenyewe kwa kauli yake kama Mwenyekiti wa Chama kesho yake akapiga ng’ombe za watu mnada yaani ng’ombe 500 zinauzwa milioni tatu” Alisema Musukuma 
Joseph Msukuma aliendelea na msimamo wake :
“Nataka nikwambie sisi Wasukuma sasa tumeamua na ninazungumza uelewe tutaziroga hizo ng’ombe mtavimba matumbo mnaozila huko Dar es Salaam, haiwezekani kwanini wanunuzi watoke Dar es Salaam peke yake yaani leo siku ya mnada watu wametoka na malori Pugu wamejuaje kama wanakuja kushinda kwenye minada. Mnatukamatia ng’ombe hivi hii serikali imekosa sehemu ya kukusanya hela mpaka mkanyang’anye ng’ombe za wafugaji haiwezekani Mh. Maghembe”

from Blogger http://ift.tt/2rU2mDF
via IFTTT


Noma Sana Aisee..Nay wa Mitego Mikononi mwa Kamanda Sirro..!!!

Rapper Nay wa Mitego amehamishiwa katika kituo cha kati cha polisi jijini Dar es Salaam kutoka Mvomero, Morogoro alikokuwa ameshikiliwa na polisi kuanzia asubuhi ya Jumapili, March 26.
Taarifa hiyo imetolewa na mwanasheria maaarufu nchini, Peter Kibatala.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2onNdI9
via IFTTT


Kimenukaa..Siku Chache Baada ya Kutoa Wimbo Unaoiponda Serikali,Nay wa Mitego Akamatwa na Polisi..!!!

Nay wa Mitego amedai amekamatwa na polisi wilayani Mvomero, Morogoro alikokuwa ameenda kwaajili ya show.
Hajasema sababu ya kukamatwa kwake lakini watu wanahisi ni kutokana na wimbo wake Wapo ambao umemkosoa vikali Rais Dkt John Magufuli. “Nimekamatwa kweli. Muda Huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza Kazi yangu iliyo ni leta. Napelekwa Mvomelo Police,” ameandika rapper huyo mtata.
“Nawapenda Watanzania wote. #Truth #Wapo,” ameongeza.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2o5MBro
via IFTTT


Kategori

Kategori