Showing posts with label 2017 at 10:35AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 10:35AM. Show all posts
Jinsi Bilionea wa IPTL-Tegeta Escrow Alivyonaswa Airport Akitaka “Kutoroka”

Jinsi Bilionea wa IPTL-Tegeta Escrow Alivyonaswa Airport Akitaka “Kutoroka”

Haikuwa ajali, pesa ya ESCROW kupita katika bank ya kanisa katoliki, mgawo kuwafikia mapadre na maaskofu,mawaziri na vigogo wa kila namna katika nchi hii. Ili siku inapobumburuka, basi msururu wa watu ujumuishwe na kuwe na “aibu” ya kuwakamata wote waliohusika.
Harbinder Singh aliitumia njia hii pia,alijenga vituo vya polisi,alikarabati nyumba za viongozi na kuwajengea “mabangaroo” wale aliohisi watamsaidia kuukwepa mkono wa dola.Alinunua pikipiki za doria za polisi,alichangia vifaa na pesa katika mahitaji ya ziada ya jeshi letu la polisi (ushahidi wa picha upo)
Pale Airport ya Dar es Salaam,kuanzia kaunta za VIP mpaka kwenye mlango wa ndege wakati wa kuondoka,wahudumu wote na wafanyakazi walijua leo Singasinga anarudi au anaondoka.Kila alipofika Singasinga au kuondoka,aliachia “tips” bila hiyana. Kuanzia kwa askari wa uhamiaji,check in counter,polisi wa Airport,mbeba mabegi,dereva wa gari la VIP mpaka mfagizi,aliinusa pesa ya singasinga.
Hii ndio maana, Singasinga kabla ya kukamatwa, alishapenyezewa taarifa kuwa anatafutwa kwa muda mrefu ili aweze kukamatwa sababu faili la ESCROW lipo juu ya meza ya “mkuu” na ameagiza kesi ianze ila tu ni lazima hawa wahusika wawili akiwemo singasinga wakamatwe.
Siku ya Ijumaa tarehe 16/06/2017,Seth alikuwa aondoke na ndege ya shirika la ndege la South Africa,flight number SA187 inayotoka Dsm kuelekea Orival Reginald Tambo International Airport,iliyotarajiwa kuondoka saa 1535(masaa ya Afrika Mashariki).Afrika Kusini ndiyo yalipo makazi ya Seth baada ya kupata mgogoro wa kifisadi na kupata shida ya kuishi Nairobi Kenya,alihamia huko Afrika Kusini.
Siku kadhaa kabla ya safari yake ya “ghafla” ya kwenda South Africa,watu kadhaa wa “mfumo” waliokuwa wanapitiwa na mgawo wa Seth, walimtonya mpango wake wa kukamatwa na kufikishwa mahakamani. Kama kawaida yake, Seth alipitisha mgawo kuhakikisha suala hilo halitokei, kuanzia yule wa chini mpaka wa juu, kila pesa ilipokuwa inamfikia, aliikimbia kwa hoja kuwa “siku hizi sio kama zamani”, wote tutakwenda na maji.
Mpaka Ijumaa asubuhi,Harbinder na wapambe wake wakawa wamegonga mwamba katika kila kona walizopita ili kuzuia kupelekwa mahakamani,suluhisho alilopewa na watu wa “mfumo” ambao walikuwa “watii” kwake sababu ya mgawo,ni kuondoka haraka nchini na kukimbilia Afrika Kusini mpaka pale mambo yatakapotulia kama zamani.
Majira ya saa nane mchana,Seth na mwanamke mmoja,walifika eneo la VIP Terminal II tayari kwa safari ya kwenda nje ya nchi ili kukwepa mkono wa mfumo. Eneo la VIP Terminal II hutumiwa na wageni mashuhuri wanaotoka au kuingia ndani ya nchi, Marais, Wabunge,Wawaziri na viongozi wengine wa hadhi ya juu na wafanyabiashara wakubwa hupitia lango hili kwa safari zao.
Seth alikamilisha taratibu zote za safari,kama kawaida yake “tips” za “kimyakimya” zilianzia mlangoni anapoingia na VIP lounge. Kilichomstua kwa haraka ni baadhi ya “tips” zake kukataliwa na baadhi ya wahudumu,alipotoa wengine waliishia kusema tu “Asante”.
Taarifa zilishafika mahali husika,kuwa Singasinga yupo Airport tayari kwa safari,akiwa na “boarding pass” mkononi na muda wowote ataingia kwenye ndege tayari kwa safari.
Bila kutarajia,wakati amevuka vihunzi vyote,akiwa anajongea kuingia katika gari la VIP,linalotumika kuwatoa wageni wa VIP eneo la VIP Lounge kuelekea kwenye ndege,ghafla ikatokea gari nyingine,kutoka mahali kusipoeleweka,likiwa limepitia mlango wa dharula na kusimama mkabala na lango la kutokea VIP lounge.
Palepale Harbinder akaamuliwa kuingia kwenye gari hilo lililokuwa na vioo vya giza,na kuachana na benzi la VIP VAN lenye maandishi ya kampuni ya Swissport kwa pembeni,mara moja gari ikageuzwa na kupelekwa kusikojulikana,mpaka mapema Jumatatu,Seth na Rugemalila walipoibukia mahakama ya Kisutu tayari kwa kusomewa mashitaka ya Escrow.
Mchezo wa kumkamata Harbinder hakuwa mdogo,hii ni kwa sababu kwa muda mrefu Harbinder amekuwa anawatumia viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama kukwepa mikono ya dola pale anapotakiwa ama kuhojiwa au sakata lake kuibuliwa bungeni.
Safari yake ya kukamatiwa Airport akiwa tayari kuingia kwenye gari kuelekea kwenye ndege,ni matokeo ya kuvujishiwa siri kuwa anatafutwa na anatakiwa kukamatwa,hivyo uwezo wa kuizima kesi haupo zaidi ya yeye kutoroka.
Hii inatupa picha,jinsi ilivyo ngumu kwa kazi hii ya kupambana na “mapapa” aina ya Singh.Inatukumbusha kauli ya Waziri Mkuu Pinda aliposema kuwa,hawa “mafisadi” wana nguvu sana,ukiwakamata nchi lazima itikisike.
Na hakika,kukamatwa kwao,nchi imetikisika,kuanzia Kanisa Kuu la Bukoba alipo Askofu Kilaini mpaka St.Joseph Cathedral Dsm alipo Askofu Nzigilwa.Parokia ya Bikira Maria wa Rozari Makongo Juu anaposali James Rugemalila mpaka makao makuu ya bank ya Mkombozi hali si shwari.
Viunga vya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nako ni tumbo joto,kuanzia kwa mwenyekiti wa Bunge na baadhi ya wabunge hali si shwari,ofisi za RITA na Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali ni matumbo joto.
Isingelikuwa mkwara wa Magufuli,Harbinder Singh angetutoroka mchana kweupe,na watu wangejiuliza,inakuwaje mahakamani tunamuona James Rugemalila peke yake?Kuna mambo JPM yanamshinda,ila kuna mengine anaamua kiasi unasahau hata yale aliyoharibu.Kumkamata Seth haikuwa kazi ndogo,alinyakuliwa wakati abiria wengine wameshaingia ndani ya ndege,akisubiriwa yeye tu wa VIP.
Hili la Escrow tukipita salama na kushinda,tumshukuru Mungu na tumpe pongezi Rais bila itikadi.Anakumbana na nguvu kubwa sana inayomsaliti katikati ya mapambano,kuna wachache wanauza “ramani ya vita” kwa adui.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2twlkDR
via IFTTT


JAY Z Afanya Kufuru ya Pesa

JAY Z Afanya Kufuru ya Pesa

PESA INAONGEA BWANA! Huku Beyonce akiwa amejifungua salama na kukaa hospitalini kwa muda wa wiki moja na nusu, hatimaye mwanamama huyo na watoto wake mapacha, wa kiume na kike wameruhusiwa kutoka hospitalini.
Habari zaidi kutoka katika ardhi ya US inatutonya kwamba baada ya watatu gao kuruhusiwa kutoka hospitalini, mumewe, Jay Z alikwishaandaa mjengo wa kupanga wa maana uliopo Malibu ambapo watatakiwa kulipia dola 400,000 (zaidi ya milioni 900) kwa mwezi tu.
Mjengo huo wa maana upo karibu na Bahari ya Pasifiki ambapo watapata muda wa kuangalia meli na watu wakila bata lakini pia mjengo una uwanja mdogo wa ndege. Mjengo una hekari 6.3, si hiyo tu, bado mtu mzima Jay Z anaendelea kusaka mjengo mwingine wa kununua huko L.A (Los Angeles).

from Blogger http://ift.tt/2sfJQtw
via IFTTT


United watarajie nini kwa Victor Lindelof?

United watarajie nini kwa Victor Lindelof?

Kutoa kiasi cha euro 30.7m kumnunua mlinzi tena mwenye umri wa miaka 22 sio jambo dogo lakini Manchester United hawakujali na wametoa kiasi hicho cha pesa kumnunua mlinzi Victor Lindelof kutoka Benfica.
Wengine wamefurahia usajili huu huku wengine wakiuliza kwanini beki wakati tayari wana mabeki wengi, lakini kama ulikuwa hujui tu baasi jua kati ya aina wachezaji au walinzi ambao Mourinho anapenda baasi nia aina ya Lindelof.
Unaweza kuona safu ya ulinzi ya United ukiacha Eric Bailly na Dalley Blind klabu hii imekuwa na aina ya mabeki ambao wanajua tu kukaba lakini baada ya kufanikiwa kukaba wanapata tabu kujua sehemu sahihi ya kuupeleka mpira na mara nyingi wanapiga tu mipira mirefu mbele.
Lindelof pamoja na umri wake lakini ni mlinzi mwenye stamina na ana nguvu haswa na kitu cha ziada alichobarikiwa anapenda sana kukaa na mpira na kuanzisha mashambulizi kama ilivyo kwa Eric Bailly ambae nae ana nguvu na ujuzi wa kucheza na mpira.
Jarida moja nchini Ureno limeandika kuhusu mashabiki wa Benfica watakachomiss kwa Lindelof na mmoja kati ya mashabiki wanaoishi karibia na uwanja wa Benfica wa Estadio Da Luz amemuelezea Lindelof kama mchapakazi sana.
Lindelof ni mchezaji ambaye mara nyingi anawahi kufika mazoezini na ni wa mwisho kuondoka na hii ndio aina ya waoiganaji Mourinho anaowataka na kama akiwa katika kiwango alichokuwa nacho Benfica baasi hakika kuna ukuta mgumu sana unaenda kutengenezwa na Lindelof na Bailly.
Benfica walikuw wakimuita “Ice Man” kutokana na aina yake ya ukabaji wa nguvu nyingi sana na akili nyingi na inasemekana Benfica walipata ofa kubwa kutoka Italia lakini Lindelof alitaka kwenda kucheza United.
Tusubiri tuone pacha hii inavyoenda kuwa lakini ni wazi Mourinho anaonekana anataka atengeze ngome imara ya ulinzi kwani msimu uliopita haswa wakati unaanza baadhi ya walinzi waliigharimu United na Mou anajaribu kuzuia hilo lisijirudie.

 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2srntA4
via IFTTT


Kategori

Kategori