CMSA NA KIGUGUMIZI CHA TAARIFA KWA WANUNUZI WA HISA ZA VODACOM

Sheria ya Fedha 2017 inalenga kuwawezeshaje watanzania kama Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imekuwa kimya kuhusu hatma ya fedha zetu toka kufungwa kwa uuzaji wa hisa wa awali (IPO) wiki saba zilizopita?
Wengi wetu tulivunja vibubu vyetu ili kununua hisa za Vodacom lakini mpaka leo Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imekuwa kimya juu ya hatma za fedha zetu. Tuna haki ya kufahamishwa nini kinaendelea.
Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) iliongeza siku 10 za uuzwaji wa hisa (IPO) ili kuwanufaisha wageni lakini imekuwa kimya kuhusu wazawa walionunua hisa zao wiki saba zilizopita.
CMSA ijifunze kutoa taarifa kwa wakati ili kusaidia kujenga imani kwa watanzania vinginevyo IPO za makampuni mengine ya simu zitakwama.
Airtel imetanga IPO yao lakini bado kuna sintofahamu ya IPO ya Vodacom inayosababishwa na ukimya wa CMSA kuhusu ziliko fedha zetu.
Hawa CMSA wanatuchelewesha kupata gawiwo letu kutoka Vodacom. Tueleweze kitu gani kinaendelea.
Leo nimekutana na mwanafunzi ambaye ametumia akiba yake TZS 300,000 aliyoikusanya kwa zaidi ya miaka mitatu kununua hisa za Vodacom lakini hana taarifa kuhusu uwekaji huo.
Wiki saba zimepita lakini watu wote tulionunua hisa za Vodacom hatujapata ‘share certificates’ zetu. CMSA imekaa kimya. Ni haki yetu kupata taarifa kuhusu uwekezaji tulioufanya.
Nimepiga simu CMSA kuomba taarifa za IPO ya Vodacom baada ya kupata wasiwasi na ukimya wao. Nimejibiwa nisubiri wakati nimeshasubiri kwa wiki nane. Kulikoni CMSA?

from Blogger http://ift.tt/2thbH81
via IFTTT