WATOTO 2000 WAAZA KUNYWA MAZIWA SHULENI NJOMBE

.

Njombe kwazinduliwa unywaji wa maziwa
Mkuu wa wilaya ya njombe Ruth Msafiri akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Nundu kulikofanyika uzinduzi wa unywaji wa maziwa kwa watoto wa shule ya msingi.


KATIKA hatua za kupambana na Udumavu mkoani Njombe wadau mbalimbali wameanzisha miradi ya kupunguza udumavu kwa watoto kwa kuanzisha unywaji wa maziwa kwanye shule za msingi halmashauri tatu za mkoa huo.

Mradi wa unjwaji maziwa kwa watoto wa chini ya miaka kumi walioko shule kwa mkoa wa Njombe unazinduliwa kwa kuanza kwa unywaji wa maziwa kwa wototo 2000 huku malengo yakia ni kufikiwa watoto 10,000 mwezi September mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akizindua mradi huo mkoa wa Njombe unaasilimia 49.4 ya udumavu ikiwa ni mkoa wa pili kitaifa, ukitanguliwa na mkoa wa Rukwa ambao unazaidi ya asilimia 50 ya udumavu licha ya mikoa hii kuwa ya kwanza kwa uzalishaji wa vyakula kitaifa.

Msafiri anasema kuwa unywaji wa maziwa kwa watoto hao 2000 mpaka 10,000 ni sawa na asilimia chini ya mbili kwa watoto wote walioko shule wenye umri wa miaka chini ya 10.

Alisema kuwa watu wasitegemea kunyweshewa maziwa na miradi nao wajipembe kuchangia kwaajili ya unywaji maziwa kwa watoto walipo shule.

Watoto hao wananyeshwa maziwa bure mradi ambao tayari umeripiwa kila kitu na Bill and Merenda Gate chini cha taasisi ya uendelezaji wa sekta ya maziwa Afrika Masharaki (East Africa Daily Development) (EADD)

Meneja wa mradi huo Mark Tsoxo baada ya uzinduzi huo alisema kuwa sasa watoto watapata maziwa kila siku za masomo ambapo watoto watakao pata maziwa ni wakle wa shule za msingi wenye miaka chini ya 10 kwa shule za halmashauri za Njombe mji, Njombe wilaya na halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe na watoto 10,000 wanatarajiwa kunywa maziwa kufiakia mwezi Septemba.

Alisema kuwa mradi huo unampango wa kuboresha afya za watoto hao kwa kuwa muda mwingi wanatumia wakiwa shule, na vilevile ni kuboresha unjwaji wa maziwa kwa mikoa ya njanda za juu kusini na kuwafanya wananchi kunjwa maziwa yaliyo sindikwa.

Maziwa yakatayonyewa wan a watoto mashuleni yatatoka kkiwanda cha maziwa Njombe ambao wananunua maziwa kutoka kwa wananchi, Meneja wa kiwanda hicho Edwin Kidehele anasema kuwa kiwanda kimejipamba kunywesha maziwa kwa watoto hao.