Elimtaa Tv: Njombe mji kukipiga na Tanzania Prison, Prison wanamajeruhi mmoja mfahamu hapa....

TIMU za Njombe Mji na Tanzania Prison ya Jijiji Mbeya zinazo tarajiwa kucheza Jumamosi wiki hii zinaendelea na mazoezi huku waalimu wake wakisema kuwa wamejipanga vizuri kuingia katika mchezo huo Prison wakisema wanamajeruhi mmoja ambaye wanawasiwasi wa kukosa mchezo huo.

Meneja wa timu ya Tanzania Prison ya Jijini Mbeya amesema kuwa timu yake imejipanga vizuri kupambana na timu ya Njombe Mji na ina majeruhi mmoja ambaye ni Beki yao na inadaiwa mchezo huo anaukosa.

Waalimu wa timu zote mbili wakizungumza kwa nyakati tofauti wanasema kuwa wachezaji wao wapo vizuri kuingia katika mechi hiyo ya ligi kuu.

Kuhusu uwanja wa Sabasaba Meneja wa uwanja huo anasema uwaja upo vizuri na wamemaliza mapungufu waliyo yaona wakati wa majaribio.


Timu ya Njombe mji inacheza mechi ya ligi kuu ukiwa ni mchezo wake wa kwanza na timu ya Prison ilikuwa Mjini Zanzibar kwa kujipanga na ligi kuu Tanzania bara.