SHULE 18 ZAFUNGIWA NA SERIKALI KIGAMBONI

Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imeendesha zoezi la kufunga shule za msingi na awali ambazo hazina usajili katika manispaa hiyo.
Zoezi hilo limesimamiwa na Kaimu Afisa Elimu wa Manispaa ya Kigamboni, Mwalimu Mathew Komba pamoja na Wakaguzi wa Elimu katika manispaa hiyo.
Image result for WANAFUNZI
Katika zoezi la ukaguzi katika shule mbalimbali, mapungufu mbalimbali yalipatikana ambayo ni pamoja na shule kutokuwa na usajili,
madarasa machache, kutokuwa na vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu ambapo baadhi ya shule zinatumia vyoo vya misikiti au wanafunzi kujisaidia kwenye vyoo vya jirani .
Katika siku ya kwanza ya ukaguzi huo, timu hiyo imezifunga shule 18 kati ya 58 zilizobainishwa kutokuwa na usajili katika kata za Kigamboni, Vijibweni na Tungu.
Kati ya shule zilizofungwa ni Malaika Nursery School, Kigamboni English Medium School, Patmos, Montecarlos, Riziki, Taqwa, Firdaus na Meck.
Aidha, uongozi wa Manispaa ya Kigamboni imewataka wazazi kutowapeleka watoto wao kwenye shule hizo mpaka hapo watakapokimilisha taratibu walizowekewa pamoja na kupata usajili.

from Blogger http://ift.tt/2wyc0Bq
via IFTTT