Mwanamziki Diamond Video Tatu Ndani ya Mwezi Mmoja za Nini zote Hizo?

Kwanza kabisa nakupongeza sana kaka kwa kazi nzuri sana, pia mimi nishabiki wako kwa kiwango cha lami.
Sasa najiuliza kwanini umeachia video tatu kwa wakati mmoja( Fire, I miss you na Eneka) zote hizo za nini bado hujiamini? Kumbuka wewe ni msanii mkubwa sana hapa Tanzania na Africa unakimbia unaenda wapi na hizo video yaani wakati mimi natafakari single yako ya fire jinsi ilivyo nzuri mara naona single ya I miss you sijakaa sawa naona Eneka.
Mwisho kabisa naomba uachane na mtindo huu unatuchanganya mashabiki wako kaka toa single moja tupe mda wa kuenjoy na single moja kwa mda mrefu kama ulivyofanya kwa single ya Merry you.

from Blogger http://ift.tt/2vo9Tvw
via IFTTT