BAADA ya Yanga kuondolewa katika mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanatarajia kumaliza hasira zao kwenye michuano ya ndani.
Kabla ya kipigo hicho cha aibu, Yanga walipata ushindi wa bao 1-0 wakiwa nyumbani na hivyo kuhitajika kupata ushindi au sare ya aina yoyote ili kusonga mbele.
Mbali na mechi za ligi, Yanga wanarejea nchini huku wakihitaji pia kutetea kombe lao linaloandaliwa na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) maarufu Azam Sports Federation Cup ambalo tayari Azam FC, Simba na Mbao FC wameingia hatua ya nusu fainali.
Katika mashindano hayo, Yanga wanatarajia kukutana na Tanzania Prisons Mei 6, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema timu hiyo imerejea jijini kwa mafungu ambapo kundi la kwanza liliwasili jana usiku na jingine leo mchana wakitokea Algeria.
“Tunashukuru Mungu tumemaliza salama ingawa matokeo hayakuwa mazuri, tumewasili jana usiku na wengine watawasili leo mchana baada ya jana kulala Dubai,” alisema Hafidh.
from Blogger http://ift.tt/2oiabks
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2nVloLJ
via IFTTT
from Blogger http://ift.tt/2pu0KPK
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2ptYGXY
via IFTTT
from Blogger http://ift.tt/2prC1P8
via IFTTT
from Blogger http://ift.tt/2ps3Jez
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2pL2Gmo
via IFTTT
from Blogger http://ift.tt/2psun6Q
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2pbGUfj
via IFTTT
from Blogger http://ift.tt/2pt5zMl
via IFTTT
from Blogger http://ift.tt/2pvQQNA
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2oGYWEG
via IFTTT
from Blogger http://ift.tt/2pMc216
via IFTTT