Wawili wakamatwa na Nyara za serikali Njombe

JESHI la polisi mkoani Njombe linawashikilia vijana wawili wakazi wa Mkoa jirani wa Iringa wakiwa na Meno ya Tembo sita yakiwa na uzito wa kilo 13.6 ambayo walikuwa katika harakati za kutafuta wateja.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe kamanda wa polisi mkoa Pudensiana Protas alisema kuwa vijana hao wawili walikuwa na Pikipiki ambapo polisi wakiwa doria katika kijiji cha Kitandililo wilaya ya kipolisi Makambako waliwakamata vijana hao.

Kamanda Protas anawataja watuhumiwa hao kuwa ni Emanuel Lyabonga na Thomas Mhomba wakazi wa Iringa wamekamatwa na jeshi hilo wakiwa na Pikipiki yenye namba za Usajili MC 916 AWN.

"Watuhumiwa hawa walikutwa na meno ya Tembo sita yenye uzito wa kilo 13.6, wakiwa na pikipiki walikuja Wilaya ya Kipolisi Makambako wakiwa wanatafuta wateja wa Nyara hizo," alisema Protas
  
Alisema kuwa watuhumiwa hao walikutwa na pem,behizo wakiwa wameziweka katika mfuko wa salfeti wakiwa wemepeba kwenye pikikipi waliyo kutwa nayo.

Alisema kuwa watuhukiwa walikuwa katika wilaya ya kipolisi Makambako kwaajili ya kutafuta wateja kabla ya kukamatwa na jeshi hilo.

Kuhusu thamani ya meno hayo Protas alisema kuwa wanasubiri wataalamu kutoka Idara ya maliasili ili kutambua thamani yake.

Alisema kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani uchunguzi wa jeshi hilo utakapo kamilika huku akitoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Njombe kuwa nyara za serikali hakuna anaye ruhusiwa kumiliki.