WAMILIKI WA VIBANDA STENDI MAKAMBAKO WAHOFIA KUKUTWA NA YA MWANZA

WAFANYABIASHARA na wamiliki wa vibanda kuzunguka stendi ya Makambako, wamepata hofu ya kufungiwa vibanda vyao baada ya halmashauri tya mji wa Makambako mkoani Njombe  kuwapa taarifa za kufanya uhakiki wa vibada vyote katika stendi hiyo.

Wafanyabiashara hao waliambiwa na halmashauri katika mkutano wao na afisa biashara kuwa wanahitajika kufanyiwa uhakiki wa kila kibanda katika stendi hiyo na kuwapa mkataba wa malipo ya kodi ya ardhi katika eneo hilo.

Wakizungumza na afisa biashara wa halmashauri ya mji Makambako wafanyabiashara hao walisema kuwa wanawasiwasi wa kuja kufungiwa vibanda vyao baada ya uhakiki huo.

Chesco Ngweta alisema kuwa wanavyo jadili kuhusu mkataba unaotarajiwa kuwekwa baina yao na halmashauri inawajia kumbukumbu ya kile kilicho fanyika halmashauri za moja mkoani Mara.

Alisema kuwa serikali inatakuwa kuwatambua na mkataba huo upakapo letwa kwao usainiwe baada ya kuupitia na kuuelewa.

Aidha afisa biashara Carros Mwenga alisema kuwa baada ya uhakiki huo halmashauri inatarajia kuanza kujipatia ushuru wa ardhi na kuongeza kwa vibanda ambavyo havija endelezwa vinandelezwa.

Alisema kupitia uhakiki huo vibanda hivyo vitatambuliwa ambavyo vinawatu na ambavyo bado havina watu na kupatiwa watu kwaajili ya kuviendeleza.

Alisema kuwa wafanyabiashara wakikubaliana kuto kubaliana yaliyo tokea katika mikoa ya Mwanza na Mara yatatokea lakini wakikubaliana kukubaliana hakuna atakaye fungiwa katika stendi hiyo.


Wamiliki hao wanawasiwasi wa kutokea yale yaliyo tokea Kwenye stendi za mikoani ya Mwanza na Mara halmashauri kufunga baadhi ya vibanda.