WANANCHI WAMTAKA MWALIMU

WANANCHI  wa kijiji cha  Idindilimunyo kata ya  Igwachanya Wilaya ya Wangingo'mbe  Mkoa wa  Njombe walifanya maandamano baada ya mwalimu kuhamishwa na mkurugenzi bila kuwapo kwa sababu za kumuhamisha.

Wakizungumza  na Nipashe baadhi ya wananchi wa kijiji hicho  walisema walishindwa kuelewa sababu zilizo tumika  na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kumuhamisha mwalimu huyo pasipo kuwaletea mwalimu mwingine wa kuziba nafasi
hiyo.

Tatizo hilo la  walimu katika shule hiyo ya Idindilimunyo inauhaba wa walimu ambao wamestaafu mwaka jana  nakufanya tatizo kubwa la walimu katika shule hiyo.
Aidha wanachi hao wakiongozana na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Gorden Kasanga  waliulaumu uongozi wa kata ya igwachanya kuwa huenda walikula njama ya kumhamisha mwalimu huyo kupitia  Mwenyekiti wa halmashauri .

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wanging'ombe Mohamed Kasinge  aliwaonya  wananchi hao kuwa wamekiuka  kanuni na sheria zilizo wekwa  na serikali juu ya maandamano
kwani wanaweza kusababisha matatizo makubwa.
Kisinge alisema walipaswa kujadili kwanza  kabla hawajanza maandamano hayo katika ofisi ya uongozi wa kata  ya Igwachanya ili waweze kusikilizwa.

Hivyo Kisinge alisema uwepo walimu saba katika shule hiyo hakuwezi athiri taaluma katika shule hiyo huku akisema kunabaadhi ya shule nyingine zina walimu watatu lakini kiwango cha taaluma kipo juu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wangingo'mbe Amina Kiwanuka  amewataka wananchi kuyaweka kwenye mawazo yao ya kuhitaji Walimu ili halmashauri iweze kushugulikia tatizo hilo ,Alisema maandamo yamekiuka
sheria na kanuni za maandamano.