Katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii pichani Juu Dkt. Donnan Mmbando akihutubia washiriki siku ya uzinduzi
Dkt.Benson Bana akisaini kitabu cha wageni kwenye moja ya banda la maonyesho siku ya uzinduzi
Kaimu Mganga mkuu wa serikali dkt. Magreth Mhando Hapo juu akihojiwa na waandishi wa habari siku ya uzinduzi wa dawa ya ZINK na ORS inayotibu ugonjwa wa kuharisha na amoxicilini,Inayotibu ugonjwa wa nimonia
Washiriki wa warsha ya uzinduzi wakiwa katika ukumbi wa blue pear hotel jijini Dar es Salaam
Kaimu mganga mkuu wa serikali dkt.Magreth Mhando akitembelea mabanda ya maonyesho siku ya uzinduzi
Tadashi Yasuda Kutoka unicefu shirika la kuhudumia watoto duniani akionyesha dawa za Kuia kuharisha na nimonia siku ya uzinduzi
Tadashi Yasuda Kutoka Unicef shirika la kuhudumia watoto duniani akihutubia waganga wakuu wa mikoa na wilaya Tanzania bara siku ya uzinduzi jijini Dar es Salaam
washiriki katika semina ya uzinduzi wa dawa za kutibu ugonjwa kuharisha na nimoni ZINKI ORS na AMOXILIN
Baadhi ya maonyesho yaliyofanyika siku hiyo ni pamoja na onyesho la kunawa mikono kwa usasahihi kabala ya kumpa huduma mgonjwa wa kuhara
Uzinduzi wa ziora ulifanyika September,10 2015 katika hotel ya blue pear jijin Dar es salaam ulihusisha washiriki kutoa mikoa ya Tanzania bara ambao ni waganga wakuu wa mikoa na wilaya ambapo mgeni rasmi alikuwa ni katibu mkuu wizazara ya afya na ustawi wa jamii dkt.Donnan Mmbando
Akihutubia siku ya uzinduzi dkt Mmbando alisema sababu kubwa ya kuzindua dawa hizo ni licha ya kuwa zimekuwa zikitumika kwa muda mrefu ni kutokana na kuwa kwa sasa zimeboreshwa kwa kiwango kikubwa baada ya maendeleo ya ugunduzi yaliyotokana na tafiti za kisayansi
Aliwaagiza watendaji wakuu wa idara ya afya, kuhakikisha upatikanaji usambazaji na matumizi sahihi ya dawa za zinki ors na amoxilin ziora katika maeneo yao ya kazi
Alisema Amoxicillin iliyozinduliwa leo ni aina ya kidonge kinachoyeyuka haraka na ni rahisi kuihifadhi na kusafirisha pia, ukilinganisha na dawa ya zamani iliyokuwa katika chupa na ORS na Zinki zimefungashwa pamoja Aliongeza Utafiti wa hivi karibuni, umeonyesha kuwa watoto wanaoharisha wanaopata ORS ni asilimia 47; wakati idadi ya watoto wanaopata zinki iko chini kwa asilimia 4.7 pekee.
Mmbando pia alisema kuwa Tanzania imepata mafanikio makubwa katika kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano licha ya kueleza kuwa kwa sasa changamoto ni magonjwa ya nimonia na kuharisha
Dr jojina msemo kaimu mkurugezi wa kinga wizara afya na ustawi wa jamii aliwasisitiza watendaji wa afya kuhakikisha wanafanikisha upatikanaji wa dawa hizo katika maeneo yao kwa kuomba dawa hizi kwa mfamasia
Naye mkurugenzi msaidizi kitengo cha elimu ya wizara ya na ustawi wa jamii Helen semu alieza na njia inayotumika kufikisha elimu kwa jamii kuhusina na upatikanaji na matumizi ya dawa hizo kuwa ni pamoja na kutmia vyombo vya habari na njia ya simu za mkononi
Tadashi yasuda Kutoka unicefu shirika la kuhudumia watoto duniani alizungumzia ukubwa wa tatizo la ugonjwa wa nimonia na kuharisha na kubainisha mikakati ya kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kimataifa kuwa ni kuendelea kusisitiza matumizi ya dawa
kila mtoto mwenye nimonia anapashwa kupata dawa ya amoxicilini, nakila mtoto anayeharisha anapaswa kupata ORS na Zinki. Dkt. Thomas Lyimo, wa shirika la kuhudumia watoto UNICEF Alieleza namna wadau mbalimbali wakiwemo UNICEF, watakavyoshiriki katika kuhakikisha dawa hizi zinamfikia kila mtoto anayestahili