Na Andrew Chale-modewjiblog
Wadau wa Mkoa wa Shinyanga wameombwa kujitokeza kwa wingi kumpigia kura Nassib Fonabo ambaye ni mwakilishi pekee anayeiwakilisha Mkoa katika shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search (BSS) kwa mwaka huu wa 2015.
Fonabo ambaye anatumia namba BSS 103, Ambapo unaweza kumpigia kura kwa wingi kwa kuandika BSS103 kwenda namba 15522. Kumpigia kura kwa wingi Fonabo zitamwezesha kijana huyo kuwa na nafasi nzuri ya kuibuka na ushindi kwani anakipaji cha pekee ikiwemo kuimba na kupiga gitaa.
Kwa upande wake, Omamy Omary kutoka Ommy Fashion Omary anasema: “ Shytown tusimame imara tumpigie kura Home boy. Ye akipata ni faida kwa wote. Heshima iludi home mazee #mwambienamwenzio”
Jumla ya washiriki waoshoriki BSS 2015, ni 20 huku kila mmoja akiwania kitita cha donge nono kutoka kwnye shindano hilo linaloendeshwa na Kampuni ya Benchmark Production kwa udhamini wa Salama Condom pamoja na kampuni ya Coca-Cola ikiwa na kauli mbiu ya Jukwaa ni Lako kuwa Original.