Afisa Mtendji Mkuu wa Shear illusions mama Shekha Nasser, akiwaeleza jambo washiriki wa Semina ya Ujasiriamlai ( hawapo pichani) Namna ya Kujitangaza kwa Kutumia njia mbalimbali, kuwahudumia na kuwajali wateja wao.Semina hiyo iliyo chini ya Manjano Foundation ina lengo la kuwajengea uwezo wana wake kujikita kwenye biashara hasa kwa kutumia Vipodozi vya Luv Touch Manjano anayeshuhudia ni Mkufunzi wa Maswala ya Biashara Ndugu Felix Maganjila.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa makini mada Mbalimbali zinazojadiliwa kwenye semina hiyo.
Mafunzo ya Ujasiriamali Phase II ya Wanawake kupitia Vipodozi vya LuvTouch Manjano yameingia siku ya tatu leo ambapo Mkufunzi wa Maswala ya Biashara Ndugu Felix Maganjila ametoa mada kuhusu namna ya kutafuta wateja na njia mbalimbali za kuuza bidhaa.Washiriki walipata nafasi ya kwenda kutafuta masoko (Marketing Research) maeneo tofauti ya Jiji la Dar es salaam pamoja na kuangalia changamoto kubwa za namna ya kuuza bidhaa zao kwa wateja wa Luvtouch na namna bora ya kuwashawishi wakazi wengine kutumia kipodozi pendwa cha LuvTouch Manjano.
Mkufunzi wa Masuala ya Biashara Ndugu Felix Maganjila akieleza jambo namna ya kuendesha biashara kwa washiriki hao.
Waliweza kuwaelezea wateja wapya kuhusu ubora wake pia kuwa wazalendo na kuunga kwa kutumia bidhaa za LuvTouch ambayo ni bidhaa ya kwanza na ya pekee ambayo ni Make-up brand ya Kitanzania inayozalishwa na Shear illusions inayomilikiwa na mzalendo mama Shekha Nasser. Baadhi ya washiriki waliopata fursa ya kufanya mauzo maeneo mbalimbali walifanikiwa kuuza bidhaa za LuvTouch Manjano.
Kwa Upande wa Afisa Mtendji Mkuu wa Shear illusions mama Shekha Nasser amewataka washiriki wanapoanzisha biashara zao na kujikota katika tasnia ya vipodozi ni muhimi hao kujitangaza ipasavyo kwa kutumia njia mbalimbali za bei nafuu maana bila matangazo hakuna biashara.
Washiriki wa semina hiyo wakifurahiya jambo.