Na Andrew Chale, modewjiblog
(Dar es Salaam)- Ndani ya masaa 24 baada ya kuachiwa kwa kibao kipya cha Msanii maarufu wa Bongo fleva nchini, Roma Mkatoliki ‘Roma Tongwe’ wimbo wa Viva Roma Viva’, tayari msanii huyo ametishiwa na kuonywa vikali na mamlaka husika kwa madai kuwa wataufungia.
Modewjiblog iliweza kushuhudia posti ya msanii huyo iliyonukuliwa kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo ile ya twitter na Instagram, facebook na Whatsapp, kwa kile kilichoelezwa na msanii huyo kutishiwa kufungiwa kwa wimbo wake huo. Hata hiv yo Roma Mkatoliki hakufafanua ni mamlaka ama idara gani inayotaka kumfungia kwa wimbo wake huo hali iliyosababisha maswali kwa wadau wa burudani huku kila mmoja akiwa na shahuku ya kuusikiliza wimbo huo kiasi cha kutakiwa kufungiwa.
Aidha, modewjiblog imeweza kushuhudia watu mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii wakiwa na shahuku ya kupata kuusikiliza wimbo huo ambao hadi sasa ndio wimbo pekee uliosambaa kwa watu wengi ndani ya muda mfupi kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Whatsapp na blog.
Moja ya ujumbe wa Roma ambao umeweza kusambaa katika kurasa mbalimbali za kijamii kwa karibu ya watanzania wengi huku wengine wakienda mbali na kuhoji mamlaka kuzifungia nyimbo zenye mlengo wa ukombozi kama huo.
Waweza kuusikiliza wimbo huo hapa chini: