Kuna machizi kati ya viongozi wa Mtaa ya Njombe Mjini


HALMASHAURI ya mji Njombe inadaiwa kuwa na viongozi wa serikali za mitaa machizi (wasio na akiri nzuri) kutokana na baadhi yao kushindwa kushiriki shughuli za mwenge na usafi wa mazingira.

Akizungumza katika baraza la madiwani la mwisho mwenyekiti wa halmashauri ya Njombe Mjini, Edwin Mwanzinga, alisema kuwa wenyeviti wa mitaa licha ya kupatiwa semina wanaenda kinyume na kile walicho kubaliana katika semina hiyo.

Alisema kuwa wenyeviti wengi ambao mwenge wa Uhuru ulipiya katika mitaa yao hawakuudhulia katika maeneo yao ambayo kulikuwa na udhinduzi.

Alisema kuwa kuna mwanasiasa alitaka wenyeviti hao kupimwa akili zao kutokana na kuonikana hawana akili nzuri katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.


alisema kuwa licha ya viongozi hao kususia katika Mbio za mwenge wake kuwa wakiwataka wananchi kuto changia michango ya taka na kusababisha halmashauri kushindwa kutekeleza usafi wa wazingira.

"Kunasiku niliingia kwa mkurugenzi nilikuta kunabarua inayo mtaka mkurugenzi kwenda kuwapima akili wenyeviti wa mitaa kwa kuwa wanaonekana hawana akili nzuri, kweli naona kuna wenyeviti wa mitaa ni machizi akili zao ni ndogo kuliko za kuku," alisema Mwanzinga

Alionheza kuwa anamuombea diwani wa Njombe Mjini kupitia Chadema Agrey Mtambo kurudi tena madalakani ili kuwanyoosha wenyeviti wa mitaa kupitia chama chake ili kuwapa semina za uongozo na atafadhili semina hizo ili halmashauri isonge mbele.

Akijibu hija hiyo diwani Mtambo alisema kuwa katika mikutano ya kata ya maendeleo (Kamaka) aliwataka viongozi hao kushiriki katika mbio za mwengi na kukubaliana huku akisema kuwa alitumia kauli ya kawaida kwa kusema kuwa mgeni akifika kwako unatakiwa kuwapo nyumbani ili kujua atafanya nini.

"Mwenyekiti wenzangu hawa niliwaambia wafike katika maeneio yao ambayo kutapitiwa na mbio za mwenge ili kujua nini kinajili, nilitumia kauli rahisi tu kuwa mgeni akifika nyumbani kwako unatakiwa kufika ili kujua nini anafanya ili asije akafanya uharibifi," alisema Mtambo.

Kuhusu usafi wa mazingira alisema kuwa kulifanyika semina kwa viongozi wote na kuwaelimisha na kuiga mbinu za ilala za wananchi mtaa kwa mtaa kuchanga wao wenyewe kutoa taka lakini wanaenda isivyo, na kusema kuwa ijulikane kuwa kila mtu na welewa wake hivyo wataendelea kurekebishana.

aidha awali akifungua mkutani huo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo alisema kuwa halimashauri hiyo imeshuka kwa nafasi mbili kwa usafi kutoka nafasi ya kwanza hadi ya tatu ambayo hawakuzoea hapo awali.

Mwisho