Baadhi ya wakimbizi wakiwa wamewasili Kigoma
Wakimbizi kutoka Burundi wakisubiri huduma mbalimbali za kijamii
Hapa watoto wa wakimbizi wakijipikia Chakula , katika mazingira hatarishi
Mamia ya wakimbizi wakiwa wanatafakari hatima yao
Hii ndio hali halisi ya vyoo ambavyo vimechangia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu
Wafanyakazi wa Shirika la Oxfam wakishusha vifaa kwa ajili ya vifaa vya upatikanaji wa maji na vyoo ili kubabiliana na Kipindupindu.
Hiki ni moja ya chanzo cha maji
Wakimbizi wakiwa ndani ya Meli
Ongezeko la wakimbizi kutoka nchi jirani ya Burundi pamoja na ukosefu wa huduma za msingi ikiwemo maji safi linamaanisha kuongezeka kwa hatari ya mlipuko wa magonjwa ya kuambukizwa hasa kwa wakimbizi takribani 40,000 walioko Kagunga mpakani mwa Tanzania.
Tayari watu 20 wamethibitishwa kuwa na ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo ya Kagunga na katika kambi ya Nyarugusu ambapo wakimbizi hupelekwa kwa ajili ya makazi.
Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) limeripoti uwepo wa watu 1057 wenye dalili za kuharisha waliopo Kagunga ambapo wakimbizi husubiria usafiri wa boti zinazowasafirisha kwenda Kigoma.
Kuna uhitaji wa haraka sana wa huduma za msingi ikiwemo maji safi na vyoo. Shirika la Oxfam linafanya kazi na shirika la TWESA ili kutoa ufumbuzi wa haraka kukidhi mahitaji hayo kwani kuna uhitaji wa haraka sana wa maji safi, huduma za matibabu pamoja na vyoo.
Shirika la Oxfam tayari limeanza maandalizi ya haraka ili kuongeza upatikanaji wa maji safi na kujenga vyoo vya dharura katika kambi ya Nyarugusu ili kukabiliana na ongezeko kubwa la wakimbizi.
Inakadiriwa takribani wakimbizi 22,000 wamesafirishwa kutoka Kagunga kwenda katika kambi ya Nyarugusu ambapo wanapewa makazi ya muda mfupi katika shule na makanisa wakati mashirika mbalimbali ya misaada yakiendelea kutoa vifaa vya ujenzi wa makazi ya muda mrefu.
Huduma za matibabu katika makambi ya wakimbizi zinasua sua kutokana na ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa mbalimbali.
Uhitaji wa haraka wa huduma za msingi ni muhimu ili kuzuia ongezeko la magonjwa yanayosambaa kama kipindupindu.