UTAFITI unaonyesha kuwa kondom zinazotolewa bure katika
vituo vya afya na Hospitali hazitoki kutokana na kuto kuwa na lebo yoyote hivi
karibuni kunatarajiwa kuwekwa lebo ya Zana ili kupokelewa na kutumiwa.
Utafiti huo umetolewa na PSI Mkoani Njombe wakati wa mkutano
wa semina kwa timu ya utoaji wa huduma za afya mkoa wa Njombe kutoka katika
vituo mbalimbali vya afya na hospitali za wilaya za mkoa huo.
Akizungumza wakati wa kutoa maada katika mkutano huo
Mkurugenzi mkazi wa PSI Tanzania, Romanus Mtunge alisema kuwa utafiti
unaonyesha kuwa kondom zinazotolewa bure katika vituo vya afya na hospitali
hazichukuliwi na watu wanao enda hospitalini na kama zikichukuliwa hazitumiki.
Alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na Psi wanatarajia kuweka
lebo itakayo zitambulisha na itaitwa Zana ili kondom hizo kuchukuliwa na watu
na kutomika na kuondoka dhana potofu kwa watu wanao zichukua na kuto zitumia
kutokana nakuto kuwa na lebo.
Alisema kuwa mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa minne
ambayo imechaguliwa kupata elimu ya ufanyaji kazi wa PSI na utamulisho wa
masoko jamii ambapo shilika hilo limekuwa likitoa huduma kwa jamii kwa kufanya
biashara jamii mbinu inayo lenga kuifikia jamii kwa kufanya matangazo na kuuza
bidhaa za afya kwa bei naufuu.
Alisema kuwa ugawaji wa kondom bure umekuwa haufanikiwi
kuliko kuuza kwa bei nafuu kutokana na watu kuto penda vitu vya bure lakini bei
ya kondom zote zinazo tolewa na shirika hilo zinauzwa bei ya chini sawa na bure
ili wananchi kuziona ni zao kulizo za bure kabisa.
Alisema kuwa kondom zilizo na lebo zinachuliwa kama
zikitolewa bure kuliko zile zisizo na lebo yoyote na kuwa halmashauri
nanatakuwa kununua kondom na kuziweka katika vyoo ili ziweze kuchukuliwa huko.
Alisema kuwa kuna wasiwasi wa kuto kuwapo kwa msaada wa
kondomu kwa mwaka 2017 kutoka kwa wafadhili kwa kuwa mpaka sasa hakuna mfadhili
yeyoye aliye onyesha nia ya kujitokeza kuchangia kondom na kuwa msaada kutoka
kwa wafadhili unaisha mwaka huu 2015 mpaka 2016.
Naye mtoa maada kutoka wizara ya afya alisema kuwa ni bora
kodomu zikauzwa kwa bei nafuu kuliko zikatolewa bure kwa kuwa zikitolewa bure
mtu anaweza kuzi tuba na kuto kwenda kuzitumia.
Alisema kuwa sekta binafsi zinasaidia serikali kuboresha
huduma za afya na kufuka kwa husahihi kutokana na huduma zinazotolewa na sekta
hizo hufavya utafiti jinsi gani wanao taka huduma wanataka ziwe na kuzitoa kwa
uhakika.
Alisema kuwa sekta binafsi ndizo zinazo buni huduma bora na
kufikisha huduma sehemu serikali haifiki na kuwa katika maeneo hatarisi ya baa
na madangulo kwa kugawa huduma huko hasa ya kondom.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika mkutano huo, Katibu
Tawara Msaidizi Rasilimali watu Gidion Mwinami, alisema kuwa elimu hiyo ya
masoko jamii itasaidia kupatiwa huduma bora kwa jamii kuta ongeza matumizi ya
elimu.