Wanging’ombe
HALMASHAURI ya Wanging’ombe Mkoani Njombe imefanikiwa
kuwaandikisha Zaidi watu 80 Elfu na
kuvuka lengo la asilimia 66 za lengo ambapo kulitarajiwa kuandikishwa watu
48,000 mpaka wanapo hitimisha uandikishwaji katika daftari la kudumu la mpiga kura
kwa mfumo wa Kierekroniki BVR.
Akizungumza na Elimtaa Blog juu ya uandikishwaji katika afisa
Uchaguzi halmashauri ya Wangimbombe, Christopher Masaaka, alisema kuwa katika
halmashauri yake wamefanikiwa kuwaandikisha wananchi zaidi ya lengo walikokuwa
wamejiwekea.
Alisema kuwa halmashauri hiyo ilikisia kuwaandikisha
wananchi 48,866, na kuwa wanawake watitarajia kuwaandikisha 26, 995 na wanaume 21871
na kuwa ongezeo ni sawa na asilimia 66 na kuandikisha kwa alimimia 166.5.
Alisema kuwa zoezi hilo limefanikiwa kwa alisilimia 166 ya
lengo ambalo halmashauri ambalo ilikuwa imejiwekea na kusema kuwa hii imetokana
na mwitikio wa wananchi katika kujiandikisha.
Masaaka alisema kuwa wanauhakika wa kuwaandikisha wananchi
wote katika halmashauri hiyo kwa kuwa kadri siku zilivyo kuwa zikienda watu
walikuwa wakipungua na kuwa mpaka siku ya mwisho katika vituo watu walio
andikishwa walikuwa hawazidi watano.
Alisema kuwa kwa wale ambao watakuwa hawajajiandikisha
itakuwa ni upendo wao kutokan ana zoezi hilo kuendeshwa kwa uhuru na kuto
mrazimisha mtu na kuwa watu wote walio pika katika vitua waliandikishwa.
“Kunavituop katika kata ya Igima tulilazimika kuongeza
mashine kutokana na idadi ya watu waliyo kuwa wamejitokeza na kumaliza watu
wate walio kuwa wamefika katika vituo vya kujiandikisha,” alisema Masaaka.
Alisema kuwa halmashauri hiyo imefanikiwa kuwaandikisha
wananchi 81,491 ambapo wanaume wakiwa 36,595 sawa na asilimia 44.91 na wanaume 44896
sawa asilimia 55.09 na kuzidi lengo walilokuwa wamejiwekea.
Zoezi hilo katika halmashauri hiyo lilimalizika juzu na
takwimu za watu walio jiandikishwa kwa ujumla kutolewa jana kukiwa na hakuna
malalamiko ya mtu kuachwa bila kuandikishwa katika daftari hilo.