Bvr Yakamilika Njombe Mjini juzi

Njombe

ZOEZI la uandikishaji katika daftarai la kudumu la mpiga kura kwa mfumo wa kielekroniki Biometric Voter Registration (BVR) hii Juzi liliingia katika siku ya mwisho mkoni Njombe ambapo dalili za wazi zimeonesha kuwa idadi ya kubwa wananchi mkoni humo wameandikishwa na kupata vitambulisho vya kupigia kura


Elimtaa Blog lilitembelea katika vituo mbalimbali katika kata mili za mwisho kukamilisha zoezi hilo kwenye kata ya Njombe mjini halmashauri ya mji vikiwemo vya mitaa ya Mgendela Kwivaha na Idundilanga na kuona idadi ndogo ya watu waliosalia katika foleni na baadhi ya vituo kuto wakuta watu.

Zoezi hilo katika kituo cha Mgendela inaonesha kukamilika kwa kuwaandikisha watu wote waliotaka kujiandikisha kuwa kuwa mpaka kufikia majira ya saa saba mchana watu walikiwa wakiingia moja moja kila baada ya dakika 20 hadi nusu saa na kuwaacha waandikishaji kupata hata mda wa kuotea jua.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mgendela Kata ya Njombe Mjini, Obadia Choga mtaa ambao viongozi wengi wa serikali wamejiandikisha katika kituo hicho akiwemo na Spika wa Bunge la Tanzania Anna Makinda na Mbunge wa Njombe, mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba, na kamanda wa Polisi.

Alisema kuwa wananchi katika mtaa wake zoezi hilo limeenda vizuri licha ya wakati linaanza kuwa na watu wengi na kubaki hadi wati 100 kwa siku kutokana na kuwapo kwa mamko wa watu katika uandikishwaji.

Alisema kuwa kufikia siku ya mwisho wananchi walikuwa wakijitokeza ka uchache kukiashiria kuwa wananchi wote kujiandikisha na kuwa waandikishaji wakijitokezwa mmoja ndani ya dakika 20 hadi nusu saa.

“Zoezi hili limeenda vizuri na wananchi wamejitokeza kwa wingi na kufikia siku ya mwisho wananchi wakijitokezwa kwa uchache kukuashiria wananchi wote wakiwa wameandikishwa na watu kwa siku za kwanza  watu walikuwa wakibaki zaidi ya mia inapo fika mda wa kufunga kituo cha Uandikishwaji kitu kilicho leta hofu ya watu kuacha ifikapo siku saba ambazo hatimaye zimemalizika kukiwa na watu wachache wakijitokeza,” alisema Choga.

Choga alisema kuwa zoezi hilo kwa mtaa wake wamefanikiwa bila kukutana na watu wasiolaia wa Tanzania ambao wamekuwa wakifika katika mtaa huo na kuisha wakiwa ni wateja wa viazi na kuwa waandikishaji walikuwa makini kwa kuangalia rafuzi ya mtu.

Alisema kuwa mbali na kuto kumbana na changamoto hiyo wamekutana na changamoto ya kuwapata watu wasio wa mtaa wake ambao walielimishwa na kuambiwa wajiandikishe itakapofika katika eneo analo ishi.

Alisema kuwa pia wamekutana na wanafunzi walio na umri ulio chini ya kiwango wanacho hitajika kuandikishwa ambao wengi wao walikuwa wa shule za msingi na kukataliwa kuandikishwa na kupewa elimu ya kujiandikisha itakapo fika mdawao wa kujiandikisha.

“Mbali na kutokubali kuwaandikisha watu walio chini ya umri wa kujiandikisha yaani miaka 17 na nusu na kuendeleza lakini nimezungumza na tume kuwa kuanzia kesho (Jana) wataanza kufuatilia watakao kuwa wamejiandikishwa mara mbili,” alisema Choga.

Alisema kuwa tume imesema kuwa itawachukulia hatua za kisheria watu wote watakao kutwa wakiwa wamejiandikisha mara mbili kwa kuwapa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu ama kulipa pesa isiyo pungua milioni 5.

Alisema kuwa kuna watu wanao tamani wakipita kitambulisho hicho wanatamani kupata na kingine hivyo wamemakini kwa kuwa kuna sheria itakayowabana kutokana na hilo.

Kwa upandewake msimamizi wa uandikishwaji halmashauri ya mji Njombe Swiga Sanke alisema kuwa kwa upande wa takwimu za watu walio andikisha katika halmashauri yake zinatolewa na tume na hivyo hata tadhimini haitatolewa.

“Kuhusi watu walio andikishwa kwamba ni wangapi mimi sihusiki wanao husika ni tume,” alisema Sanke.