Al Shabaab inaendelea kuwasajili Wakenya


Al Shabaab inaendelea kuwasajili wapiganaji katika miji mikuu nchini Kenya kulingana na ushahidi uliobanika na BBC
Huku ujenzi wa ua utakaotenganisha Kenya na Somalia ukianza kwa madhumuni ya kuwakomesha wanamgambo wa Al Shabaab kutoishambulia Kenya,
shirika la BBC limepata ushahidi kuwa kundi hilo lenye makao yake nchini Somalia linaendelea kuwasajili wanachama wapya katika miji mikuu ya Kenya.
Katika mji wa Isiolo ulioko Kaskazini Mashariki mwa Kenya, takriban vijana barubaru 26 wametoweka makwao.
BBC imebaini kuwa vijana hao wamewapigia wazazi wao simu wakiwaarifu kuwa tayari wamejiunga na wanamgambo wa Al Shabab.
Nusu ya wazazi wao wameripoti kutoweka kwao kwa vyombo vya usalama .
BBC imebaini kuwa vijana hao wamewapigia wazazi wao simu wakisema kuwa tayari wamejiunga na wanamgambo wa Al Shabab
Asilimia kubwa ya wale waliokaa kimya wanahofia kudhalilishwa na maafisa wanaopambana na ugaidi nchini Kenya .
Ilikuwashawishi wakenya kujiunga na serikali kutambua wafuasi wa kundi hilo waliotangamana na jamii, serikali ya Kenya imetangaza
msamaha kwa wakenya waliojiunga na Al Shabaab maadamu watajisalimisha kwa vyombo vya dola katika kipindi cha siku 10 zilizotolewa.
Matukio haya yanawadia takriban majuma mawili tangu wapiganaji wa kundi hilo kuivamia chuo kikuu cha Garissa na kuwaua takriban wanafunzi wakristu 150.
Serikali ya Kenya baadaye ilitangaza kuwa kiongozi wa wapiganaji hao alikuwa ni Wakili mkenya.
Kundi hilo lilivamia chuo kikuu cha Garissa na kuwaua takriban wanafunzi 150
Usajili huu unaoendelea unatizamwa na wachanganuzi wa maswala ya kiusalama kama mbinu mpya na ya kuhofiwa.
Ukweli ambao umewaogofya wabunge na maafisa wa usalama nchini humo.
Hata hivyo mmoja wa viongozi wa kiislamu wanaoheshimiwa nchini Kenya Sheikh Abdullahi Salat, ameonya kuwa hofu ya jamii dhidi ya polisi na shauku huenda ikahujumu jitihada hizo.
Serikali imepuzilia mbali maoni hayo ikidai kuwa ni kisingizio tu.