Matukio 10 makuu baada ya mauaji Garissa


Polisi wakishika doria katika eneo la tukio Garissa
Familia za wanafunzi 142 kati ya watu 148 waliouawa katika shambulizi la kundi la wapiganaji wa Kiislamu Al Shabaab katika chuo kikuu cha Garissa wameruhusiwa kuchukua miili ya wapendwa wao.
Familia zimeanza harakati za safari ya mwisho ya wapendwa wao baada ya serikali ya Kenya kuwaruhusu kuzichukua miili kutoka kwenye hifadhi ya maiti ya Chiromo jijini Nairobi.
Huu hapa mukhtasari wa matukio baada ya shambulizi hilo.
Shambulizi lilipokuwa likiendelea
1.Shambulizi
Takriban wanamgambo 5 wa kundi la wapiganaji wa Kiislamu Al Shabaab washambulia chuo kikuu cha Garissa alfajiri.
Waliwapata wanafunzi wakiwa wamelala.
Waliingia chuoni baada ya kuua walinzi wawili langoni.
Walionusurika wanasema kuwa wavamizi hao waliwabagua wanafunzi waislamu na kuwaua wakristu.
Misa ya wafu huko Garissa
2.Uhuru ahakikisha taifa
Serikali ilitangaza kuwa watu 70 walikuwa wameripotiwa kuuawa na wengine 79 kuripotiwa kujeruhiwa.
Waziri wa usalama wa taifa generali mstaafu Joseph Nkaissery alitangaza idadi ya waliouawa kuwa ni 148 na kusema kuwa operesheni ilikuwa imekamilika
3.Idadi ya waliouawa yatangazwa
Wanafunzi 500 wameokolewa na maafisa wa usalama
Rais Uhuru Kenyatta ahutubia taifa na kutuma risala za rambirambi kwa wale waliouawa.
Serikali ilionyesha hadharani miili ya wanamgambo waliouawa na kuonyesha picha ya raia mmoja kutoka Tanzania aliyekamatwa.
Jamaa ya walioathirika
Rais Uhuru Kenyatta atangaza kuwa Serikali yake itachukua hatua kali dhidi ya wakenya wanaolisaidia Al Shabaab.
Serikali yakiri kuwa mmoja kati ya washambuliaji hao alikuwa ni mwanawe Chifu wa kata ya Mandera.
Chifu huyo yamkini alikuwa ameripoti kwa polisi kuhusu kutoweka kwake mwaka uliopita.
4.Maswali yaibuka kuhusu Operesheni
Maswali yaibuka kuhusu hatua zilizochukuliwa na polisi baada ya kuarifiwa kuhusu shambulizi hilo.
Wananchi waizomea serikali kwa kutumia ndege kuwasafirisha waziri wa usalama wa taifa Joseph Nkaissery na Inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinett
huku kikosi maalum cha kupambana na magaidi al maarufu (RECCE) kikilazimika kusafiri kwa gari kwa zaidi ya saa saba.
Wanafunzi walionusurika
Kikosi hicho kilitumia chini ya dakika 15 pekee kukamilisha operesheni hiyo.
5.Makurutu 10,000
Rais Uhuru Kenyatta atangaza kuwa makurutu 10,000 wa polisi waliokuwa wamepigwa marufuku na mahakama kufuatia madai
Waliotekeleza shambulizi la Garissa watajwa
ya rushwa sasa hawatakuwa na budi ila kuingia katika chuo cha mafunzo ya Polisi ilikuimarisha idadi ya polisi na vilevile usalama wa taifa.
Mahakama ilikuwa imeharamisha kusajiliwa kwao kufuatia madai ya rushwa katika usajili.
6.Waliotekeleza Shambulizi watajwa
Raia wa Kenya Mohamed Kuno kwa jina jingine Mohamed Dulyadin,atajwa kuwa ndiye mshukiwa mkuu.
Serikali ya Kenya imetoa ruzuku ya shilingi milioni 20 za Kenya yaani dola $215,000 za kimarekani.
Taifa lahuzunika
Kuno aliwahi kuwa mwalimu katika eneo la Garissa kabla ya kustaafu na kujiunga na kundi hilo.
Mwengine aliyetajwa ni wakili Abdirahim Abdullahi aliyeongoza uvamizi huo.
Wanafunzi walionusurika Rais Uhuru Kenyatta aonya kuwa wale wanaoendeleza sera za Al Shabaab wako miongoni mwa wakenya.
7.Maiti yaletwa Nairobi
Manusura waliopatikana wamelala
Maiti ya wahanga wa mauaji hayo yaletwa mjini Nairobi kwa ndege za kijeshi.
Wale walionusurika pia wasafirishwa kwa msafara wa mabasi hadi mjini Nairobi.
Kituo cha kuwapokea waathiriwa wa mauaji hayo na jamaa zao kinaundwa katika uwanja wa michezo wa Nyayo mjini Nairobi.
Wale walionusurika pia wasafirishwa kwa msafara wa mabasi hadi mjini Nairobi
Orodha ya wanafunzi waliouawa na wale waliojeruhiwa inapachikwa katika lango la uwanja wa Nyayo.
8.Serikali yafunga miundo mbinu ya uchumi wa Al Shabaab
Serikali ya Kenya yatangaza orodha ya mashirika kumi na tatu na akaunti za watu
binafsi wapatao 86 wanaoshukiwa kuhusika na ufadhili wa kundi la kigaidi la Al Shabaab Garissa.
Akaunti za watu hao ambao zimesitishwa ni baadhi ya watu waliokuwa katika orodha ya serikali ya Kenya ambao walikuwa wakifuatiliwa mienendo yao.
kampuni 13 za ubadilishaji na usafirishaji wa fedha nazo zimefungwa.
Maafisa wa Polisi wakishika doria
Jamii ya wasomali yalalamikia hatua hiyo ikisema ni mtego ambao umenasa waliokuwemo na wasiokuwemo.
9.Utambuaji wa maiti Chiromo
Shughuli ya utambuaji wa maiti yaanza huku familia nyingi zikitatizika kutambua miili ya wapendwa wao kufuatia kuharibiwa kabisa kwa miili.
Miili mingi ilikuwa na majeraha ya risasi kichwani.
Serikali ya Kenya yalazimika kutumia mashine maalum ya kutambua chembechembe za damu za DNA ili kuharakisha utambuzi wa miili.
Dukuduku zaibuka kuhusiana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wazazi ambao wamekosa miili ya wapendwa wao.
Muungano wa walimu na wafanyikazi wa vyuo vikuu (UASU) yadai kuwa takriban wanafunzi 166 hawajulikani waliko.
10.Uhuru aomboleza
Rais Uhuru Kenyatta aliwaandikia familia ya wahasirika wote barua ya kuomboleza
Rais Uhuru Kenyatta jana aliwaandikia barua kila familia iliyopoteza mpendwa wao.
Wote walioathirika walipewa shilingi laki moja za Kenya,Jeneza na gari la kusafirishia maiti hadi makwao.
Makumi ya raia wa kigeni wakamatwa kote nchini kufuatia msako mkali unaoendelea

imeandaliwa na bbc/swahili