Wapiga kura milioni 13 kuchagua rais Sudan


Wagombea 15 wanaoshindana na Bashir kwenye uchaguzi huo
Uchaguzi Mkuu nchini Sudan unafanyika wiki hii, huku Rais wa sasa Omar Al Bashir akitarajiwa kushinda. Vyama vya upinzani vimesusia uchaguzi huu vikidai hautakua huru na haki.
Bashir ndiye kiongozi pekee wa nchi aliyewekewa waranti ya kukamatwa na mahakama ya kimataifa ya ICC.
Takriban wapiga kura milioni 13 watakuwa wakimchagua Rais na wabunge 450.
Matokeo yanatarajiwa kutangazwa Aprili 27.
Huu ndio utakaokuwa uchaguzi wa kwanza tangu Sudan Kusini ijitenge 2011.
Huu ndio utakaokuwa uchaguzi wa kwanza tangu Sudan Kusini ijitenge 2011
Vyama vingi vya upinzani vinasusia uchaguzi huo kutokana na kile vinavyodai kuwa ukandamizaji wa kisiasa unaoendeshwa na rais Omar al Bashir.
Rais Bashir alifanya kampeni kubwa , akihutubia mikutano ya hadhara sehemu tofauti za taifa hilo kubwa.
Vyama vingi vya upinzani vinasusia uchaguzi huo ikiimanisha kuwa bashir na chama chake wana uhakika wa kushinda.
Wagombea 15 wanaoshindana na Bashir kwenye uchaguzi huo hawana uwezo mkubwa na wengine hata hawajulikani kote nchini Sudan.
Wagombea 15 wanaoshindana na Bashir kwenye uchaguzi huo
Vyama vya upinzani vimesusia uchaguzi licha ya chama kimoja kikubwa kuwa na wagombea wa ubunge baada ya kudai kuwa itakuwa vigumu kwa uchaguzi huo kuwa wa haki.
Tangu mwaka uliopita wanasiasa kadha wa upinzani wamekamatwa huku vyombo vya habari vikiwekewa masharti makali.
Pia kuna mizozo katika majimbo la Darfur, Kordofan kusini na Bule Nile.
Nchi za magharibi zinaonekana kupendelea upinzani lakini rais Bashir ana matumaini kuwa ushindi wake utakubaliwa barani Afrika na kwenye nchi za kiarabu.