Watu wapatao kumi na watatu wameuawa katika katika mashambulio mawili yaliyotokea kwa pamoja katika rasi ya Sinai nchini Misri.
Watu saba waliuawa na arobaini na wanne kujeruhiwa wakati bomu lililokuwa limetegwa katika gari kufyatuka katika kituo cha polisi katika mji wa al-Arish.
Mapema, saa chache bomu lililokuwa limetegwa pembeni mwa barabara liliwaua askari sita katika mji wa Sheikh Zuweid.
Kundi linalojiita "Province of Sinai" yaani Jimbo la Sinai --ambalo linachukuliwa kama tawi la Islamic State -- limesema ndilo lililofanya mashambulio yote mawili.
Wapiganaji wa kundi hili wamesema wanalipiza kisasi dhidi ya serikali ya Misri ambayo inawasaka wafuasi wa rais wa zamani wa Misri aliyeondolewa madarakani, Muhammad Morsi.