CHAMA cha Demokrasia na Manendeleo (Chadema) Mkoani Njombe kimesema kuwa hakita shiriki kuipigia kura katiba pendekezwa ambayo inatarajiwa kutangwazwa siku ya kuipigia kura wakati wowote huku wakiunga mkono kauli za viongozi wa dini kupinga mahakama ya kadhi na kauli ya Gwajima.
Akizungumza na katika uzinduzi wa albamu ya kwaya ya Ebeneza, kanisa la Pendekosti Igosi la Mkoani hapa, Mwenyekiti wa Chadema Mkoani Njombe Rafael Lulandala, alisema kuwa Kamati kuu cha yama hicho imesema haita husika kabisa katika kupigia kura katiba pendekezwa tofauti na viongozi wa dini kuwashawishi wananchi wake kupiga kura ya hapana.
“Mimi nilipo kuwa kanisani ninakosali mchungaji wakati anasoma tamko la jukwa la maasikofu la kupigia kura ya hapana kwa wakristo wote haliendi mbali sana na tamko la chama chetu la kuto piga kabisa kura na tutapiga kampeni za kuto shiriki katika majukwaa yetu,” alisema Lulandala
Lulandala aliongeza “Najua ni kwa sababu kuna vitu ambavyo maaskofu hawavitaki viwemi katika katiba ndio maana wanawaanbia mpige kura ya hapana ili iludi tena bungeni ikatengenezwe upya,”.
Alisema kuwa Chadema haita husika kabisa katika mchakato wa kupigia kura katika Katiba bendekezwa na badala yake watasuburi matokei na ikipita watakana katiba hiyo.
Alisema kuwa wakishiriki kupiga kura maanayake ikipita wata kuwa wamehusika lakini wameshindwa kuizuia.
Alisema kuwa anaungana na kauli ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, licha ya kuwa naye anamapungufu yake lakini katika mahubili yake alisema amemuelewa maana yake lakini alikosea katika ufikishwaji wa ujumbe.
“Kiongozi aliye toa kauli yake nakubaliana na ye licha ya kuwa naye anamapungufu yake lakini ukifuatilia mahubili yake yalikuwa ya msini licha ya ufikishwaji wa ujume haukuwa wa usahihi sana, katika mahubili yake anasema mahakama ya kadhi inaweza kusababisha vida ya kidini kama dini moja ikitoa hukumu kwa mtu wa dini nyingine,” alisema Lulandala.