FREEMASON WATUA KANISA LA GWAJIMA


Stori: Waandishi Wetu
WATU wanaodaiwa kuwa ni wa imani ya Freemason wametua ndani ya ibada katika Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima, Uwazi lina ‘ei tu zedi’ ya tukio hilo. Kwa mujibu wa chanzo chetu, Freemason hao wawili waliingia kwenye ibada hiyo iliyofanyika Februari 23, mwaka huu ndani ya kanisa hilo lenye makao makuu yake katika Viwanja vya Tanganyika Peckers, Kawe jijini Dar wakiwa na mfuko wa rambo wenye vitu mbalimbali vikiwa na alama zao. GWAJIMA MADHABAHUNI
Habari zilidai kwamba wakati neno likiendelea kunenwa na Mchungaji Gwajima, watu hao walifunua mfuko huo ambapo baadhi ya waumini waliokuwa karibu yao walihoji kulikoni kuwa kwenye ibada na vitu vyenye viashiria ya Freemason. “Wengine…
GPL