Wananchi wajitokeza kujenga nyumba za waathirika wa Mvua

Baadhi ya wanachama wa CCM wilaya ya Tabora mjini wamejitokeza kusaidia kuwajengea nyumba waathirika wa mvua kubwa zilizonyesha mkoani mjini humo na kubomoa zaidi ya nyumba 24 na kusababisha kaya thelathini kukosa makazi katika kijiji cha Tumbi.
Wanaccm hao wameunga mkono wito wa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini Bw.Moshi Abrahamu maarufu Nkonkota, na kulazimika kuchangia nguvu zao kuwasaidia watu walioathirika na mvua kubwa iliyonyesha siku ya mkesha wa Sikukuu ya Krismas ambapo baadhi ya watu katika tukio hilo walikosa makazi baada ya nyumba zao kubomoka.
Bibi Joha ni mmoja kati ya watu walioathirika na mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali na kusababisha kubomoa nyumba yake hapa anaeleza furaha yake baada ya kupatiwa msaada na wanaccm hawa waliojitoa mstari wa mbele kumtafutia sehemu ya kusitiri maisha yake kwa kumjengea kibanda kingine kwa ajili ya makazi.