JKT Watakiwa kuendeleza kilimo cha kisasa na kuwa darasa kwa wakuluma Kigoma

Licha ya kuwepo kwa mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa vijiji sita wilayani Kasulu na Kambi ya JKT kikosi cha 825 Mutabila, Mkuu wa mkoa wa Kigoma Luteni Kanali mstaafu Issa Machibya amekitaka kikosi hicho kuendelea na mipango ya kilimo cha kitaalamu kitakachokuwa na shamba darasa kwa ajili ya kunufaisha wakulima wa vijiji jirani na vijana katika mafunzo na kuleta tija katika maisha yao.
Wito wa mkuu wa mkoa umetokana na kauli ya mkuu wa wilaya ya Kasulu Dany Makanga katika mahafali ya pili ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi kwa vijana 1110 wa oparesheni miaka 50 ya uhuru kundi la pili kwa mujibu wa sheria na kwamba wananchi wa vijiji wamevamia eneo la kikosi kwa kilimo mkuu wa idara ya kilimo kikosini hapo Meja Thomas Gairo akieleza kuwa vijana wameiva kwa stadi za kilimo.
Awali kaimu mkuu wa kikosi hicho Meja George Kazaula na Mwakilishi wa mkuu wa JKT nchini Meja Abdulrahman Dachi wamesema vijana hao ni nguzo ya taifa hili katika ulinzi, usalama na uzalishaji mali.