Vijana, Wanawake, Walemavu Watakiwa kuunda vikundi

Chama cha Mapinduzi kimesisitiza kuwataka makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kuunda vikundi vitakavyowapa fursa ya kunufaika na uwezeshaji wenye lengo la kuwajengea uwezo wa kiuchumi na hatimaye kuondokana na umaskini.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mtwara Vijijini Alhaj Saad Kusilawe ametoa kauli hiyo, alipokutana na vikundi vya akina mama wa vikoba wa kata ya Kigamboni wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, waliokuwa wakimpongeza diwani wa kata hiyo kutokana na mchango wake wa kuimarisha vikundi hivyo.
Awali akina mama hao katika risala yao walimpongeza diwani huyo Doto Msawa kwa juhudi ambazo zimewezesha vikundi 27 vya vikoba kukuza mitaji yao, ambapo sasa malengo yao kufikia uwezo wa kukopeshana shilingi Milioni tano kwa kila mwanachama kwa mara moja, huku diwani huyo akiwasisitiza kuendeleza mshikamano