Meli yatelekezwa Italia

Walinzi wa Pwani ya Italia wamesema Meli ya Kibiashara iliyokuwa na wahamiaji wapatao 400 inaelekea kwenye Pwani ya nchi hiyo.
Meli hiyo, Ezadeen iliyokuwa ikisafiri kwa bendera ya Sierra Leone haikuwa na wafanyakazi ndani yake na imepoteza mwelekeo kwenye bahari yenye mawimbi makali Kusini Mashariki mwa Italia.
Meli za Italia zimekuwa zikitoa msaada kuwasaidia watu waliokuwa ndani ya Meli hiyo. Zaidi ya wahamiaji elfu moja wameokolewa na kuwekwa kwenye meli nyingine.
Meli hiyo ilitelekezwa bila ya wafanyakazi wala nahodha mapema wiki hii.