MKUU wa mkoa wa Njombe
Dk Rehema Nchimbi amewaomba wakurugenzi wa halmashauri kuwatambua walimu
wanaojiendeleza kimasomo kwa kuwapatia tuzo wakati
wanapofanikiwa ili kujenga mahusiano na ushawishi kwa walimu wengine
kujiunga Elimu ya juu.
Akizungumza Wakati wa hafra ya kumuaga makamu wa Chuo kikuu Huria Tanzania Tolly Mbwette katika tawi la chuo hicho mkoa wa Njombe, Dr Nchimbi alisema kuwa wakurugenzi wa halmashauri wawatamue waalimu wanao jiendeleza kwa kuwapatia tuzo na motesha ili kuwashawishi na waalimu wengine kuendelea kujitokeza kujiendeleza.
Alisema kuwa waalimu
wajitahidi kujiendeleza katika elimu ya juu na pindi watakapo jiendeleza wasihame
katika vituo vyao vya kazi kwani serikali itaanza utaratibu wa kuwaangalia
jinsi ya kuwapatia motisha, kwani serikali inampango wa kuwa na waalimu wengi
wa shule za msingi wenye elimu ya juu.
Aliongeza kuwa kwa sasa serikali
imebadilisha mfumo wa wanafunzi kujiunga na vyuo vya uallimu kwa wanao maliza
kidato cha nne hawata jiunga na vyuo vya ualimu na kuwa waliovyuoni ni hao hao
hakuta kuwa na waalimu wanao jiunga na kutoka kidato cha nne na kuwa sasa walio
kidato cha sita ndio watakao kuwa wanajiunga na vyuo vya ualimu.
“Mimi mwenyewe nilikuwaq mwalimu
nikajiendeleza mpaka sasa ni Dr. hivyo waalimu msivunjike moyo wa kujiendeleza
mjitahidi kujiendeleza kwa kujiunga na vyuo hasa chuo huria kinawapa fulsa za
kusoma wakati uko kazini, pia nanyi chuo kikuu maafari yakifanyika kila kanda
yatawapa motisha na wengine kuona wakitukiwa kwa kuvaa mashera,” alisema Dr.
Nchimbi.
Dr Nchimbi alimpongeza Profesa huyo kwa kuanzisha mufumo wa mahafali kwa wahitimu wa chuo hicho na kwamba mfumo huo unatakiwa kuboreshwa na kutumiwa kwa nyanda za juu kusini ili wahitimu wakutane kwaajili ya mahafari na kuhamasisha wengine kujiunga na chuo hicho.
Akizungumza mara baada ya
hotuba ya mkuu wa mkoa wa Njombe muagwa katika chuo kikuu huria cha Tanzania Prf
Tolly Mbwette alisisitiza viongozi wa chuo wanaobakia kuhimiza matumizi
yatehama kwa wanachuo ambapo amesema katika kipindi cha miaka ijayo
matumizi hayo yatakuwa ni ya razima kwa kila mwanachuo.
Hiyo aliwataka waalimu kujua matumizi ya
Tehama kwa kuwa serikari kwa miaka ijayo itakuwa inafundisha kwa mufumo wa Tehama
kwa lengo la kuboresha elimu ya hapa nchini na kuendana na wakati