Polisi nchini Israel imewakamata wapalestina
wasiopungua 23 katika eneo la mashariki la mji wa
Jerusalem kuanzia jana usiku hadi leo katika msako
uliofuatia miezi kadhaa ya machafuko katika mji huo
mtukufu-maafisa wa Palestina wamesema. Hata
hivyo msemaji wa polisi amesema waliokamatwa ni
watu wanne,bila ya kuwataja wengineo ambao
pengine wamekamatwa na idara nyengine za
usalama. Waliokamatwa ni wakaazi wa Issawiya na
Wadi Joz-mitaa ya waarabu katika eneo linalokaliwa
na Israel Mashariki ya Jerusalem pamoja pia na mji
mkongwe-shirika linaloshughulikia wafungwa wa
kiplastina limesema katika taarifa yake. Alhamisi
iliyopita polisi ya Israel ilimpiga risasi na kumuuwa
mpalastina anaetuhumiwa kutaka kumuuwa
mchamngu wa kiyahudi-rabbi-anaefuata nadharia
kali za kiyahudi na kusababisha mapigano makali
kati ya vijana wanaovurumisha mawe na vikosi vya
usalama vilivyokuwa vikifyetua gesi za kutoa
machozi na risasi za mpira. Kwa mujibu wa
polisi,wapalestina wasiopungua 11 wamekamatwa
tangu machafuko ya Oktoba 22 Mashariki ya
Jerusalem.
Habari Online na Elimtaa
Habari na DW.DE
Wapalestina zaidi wankamatwa na vikosi vya uslama vya Israel
Subscribe to:
Post Comments (Atom)