Mapigano makali yameripuka karibu na mji wa bandari wa mashariki ya Libya-Benghazi hii leo,pale jeshi likiungwa mkono na vikosi vitiifu kwa jenerali wa zamani,Halifa,Khaftar,lilipowashambulia wanamgambo wa itikadi kali.
Wakaazi wa eneo hilo wamesema, raia kadhaa wanauhama mji huo,wakiitika wito wa jeshi wa kuondoka katika mji huo wa bandari ambako maafisa wa kijeshi wanasema wanamgambo wa itikadi kali wamejificha baada ya zaidi ya wiki mbili za mapigano. Mwandishi wa shirika la habari la reuters anasema ameshuhudia jeshi likiweka vifaru na silaha nzito nzito katika mji huo wa pili kwa ukubwa nchini Libya.