Watu wasiopungua 24 wamefariki mashua ya
wakimbizi ilipozama karibu na mji wa Istanbul
nchini
Uturuki. Wengi wa wahanga hao ni watoto-gazeti la
Uturuki-Hürriyet likiwanukuu waokozi limeandika
katika mtandao wake wa
internet. Inakadiriwa
wakimbizi 40 walisheheni katika mashua hiyo.
Chombo hicho kimezama karibu na ujia wa maji wa
Bosporus katika bahari nyeusi. Wengi wa wakimbizi
hao ni wa kutoka Afrika na Mashariki ya kati
waliokuwa njiani kuelekea katika nchi za Umoja wa
Ulaya kupitia Uturuki. Ujia wa maji wa Bosporus
unopendwa kutumiwa na meli zinazosafirisha mafuta
na pia meli zinazosafirisha mali ghafi unaugwa
sehemu mbili mji wa wakaazi milioni moja wa
Istanbul nchini Uturuki.