Baada ya uchaguzi unaobishwa wa mashariki ya
Ukraine, ushindi unasemekana umewaendeya
viongozi wa waasi wanaoelemea upande wa
Urusi,Alexander Sachartschenko wa Donetsk na Igor
Plotnizki wa Luhasank. Wote wawili wamejikingia
wingi wa kura katika jamhuri zilizojitangaza wenyewe
mashariki ya Ukraine. Kwa kuitisha uchaguzi huo
waasi wanataka kuimarisha msimamo wao katika
majimbo ya Donetsk na Luhansk na kudhibitisha
uhuru wao dhidi ya serikali ya mjini Kiev. Nchi nyingi
za magharibi zinautaja uchaguzi huo kuwa si halali.
Urusi imeshasema itaheshimu matakwa ya wakaazi
wa maeneo hayo yaloyoasi. Waziri wa mambo ya
nchi za nje wa serikali kuu ya Ujerumani Frank-Walter Steinm eier ameitolea wito serikali ya Urusi
mjini Moscow isichangie kuzidi kukorofisha hali ya
mambo nchini Ukraine. Katika mahojiano na DW,"
waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani
amesisitiza kwamba, Uchaguzi wa Mashariki ya
Ukraine ni kinyume na mwongozo wa makubaliano
ya Minsk.