WAKULIMA wa chai Nyanda za juu
kusini na Tanzania kwa Ujumla wanatarajiwa kunufaika na mfumo wa kuweka
kumbumbu zao katika mtandao na kuwa wazi kwa kila mkulima na bodi ya chai.
Akizungumza na Waandishi wa
habari wakati wa kutoa mafunzo kwa wawakilishi wa viwanda vya chai,
wawakilishi wa wakulima, na vyama vya wakulima kuhusiana na mfumo huo, afisa
mkaguzi mkuu, Bodi ya Chai, Fahari Marwa, amesema kuwa mfumo huo utapunguza
matatizo mbalimbali yaliyo kuwa yakitokea baina ya wakulima na viwanda.
Amesema kuwa mfumo huo inatarajiwa
kutatua migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza baina ya wakulima na viwanda hasa
makato ya mikopo ya pembejeo, na malipo ya pili kwa mkulima.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya
Njombe Sarah Dumba amesema kuwa mfumo huo utasaidia kuondoa matatizo ambayo
yamekuwa yakitokea mara kwa mara na utaepusa manungu’uniko kwa wakulima.
Amesema kuwa wakulima wamekuwa
wakiyakosa malipoi ya pili ambapo malipo hayo yamekuwa wakiliwa na wajanja
ambao wapo katikati ya wakulima na viwanda katika vikundi vyao.
