Pole Prof. Jk (Taarifa zinasema Rais Jk anaendelea vizuri) Elimtaa Blog Enaendelea kumuombe

Rais Prof. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepumzika kwenye hoteli maalumu
baada ya kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore
Maryland alikotolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji
wa Tezi Dume wiki iliyopita..Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena
hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na
ushauri.
 


Rais Prof. Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns
Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika
mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita.Rais Kikwete
anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa
maendeleo ya kidonda na ushauri .Kulia kwake ni Daktari wa Rais
Profesa .Mohamed Janabi
  (Picha na  Freddy Maro)