Mdh: Yapania kupambana na Ukatili wa kijinsia

UPIMAJI  wa vina saba unatarajia kupambana na wanao husina na ukatili wa kijinsia ukiwemo wa ubakaji kwa watoto na wakinamama, hapa nchini na vituo 65 mkoani Dar es salaam vinatoa huduma kwa jamii. Akizungumza na waandishwa wa habari mkoani Njombe,  Meneja wa Huduma za Jamii wa Management and development for Helth (MDH) katika wiki ya Ukimwi Duniani, Dr. Irene Lema jana alisema kuwa upimaji wa vinasaba utasaidia kuwatambua wanao fanya ukatili wa kijinisa.
Alisema kuwa MDH ina mpambo wa kutoa huduma ya upimaji wa vina saba kwa watakao hitaji hapa nchi kwaajili ya kuwabaini wanaofanya ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake.
"Upimaji wa Vina saba unasaidia kubaini mtu halisi aliye fanya ukatili wa kijinsia, pia inashauriwa mtu aliyefanyiwa ukatiki wa kijinsia anatakiwa kutoa taarifa mapema ili kusaidia katika utatuzi wa tatizo lake," alisema Lema.
Alisema kuwa wamekuwa wakifanya kwa ukaribu na Wizara ya afya kuhakikisha huduma mbalimbali ikiwemo ya vina saba inatolewa kwa jamii bila kuwapo kwa kikwazo.
Lema alisema kuwa sasa wanaendesha mafunzo katika mikoa mbalimbali hapa nchini na kuwa wanaanza kutoa mafunzo juu ya utumiaji wa vina saba na kuwa wanata kuifikia mikoa ya Dar es salaam, Iringa, Mbeya, Njombe na Mara.
Aliongeza kuwa wanataka mfumo huo kuwa endelevu na huduma hiyo kuwepo kwa mkemia mkuu na kuwa watahakikisha katika kafunzo hayo kila mkua unakuwa na wataalamu wa kutambua vina saba.
Taasisi hiyo isiyo kuwa ya kiserikali ambayo imeona umuhimu wa kutumika kwa Vinasaba kwa watendewa ukatini na kuitaka jamii kutoa taarifa mapema kwa mtu aliyefanyiwa ukatili na kupatiwa huduma kwa wakati itasaidia jamii kujua kwa urahisi vinasaba.

Aidha Lema aliongeza kuwa ukatili wa kijinsia ni moja ya vitu vinavyo ongoza kwa kuwapo kwa maambukizi ya Ukimwi hapa nchini na mkua wa Dar es Salaam kuoinmgoza kwa ukatili wa kijinsia.