Usajiri wa Siraha waanza

Kuendelea kwa Kenya kuzuia utoaji leseni za kumiliki silaha kwa raia kumeibua mjadala kwa umma, huku waombaji wakihoji uhakiki huo wa mchakato wa utoaji leseni unachukua muda mrefu na kuhatarisha maisha na mali zao.
  • Wanaume walioshikiliwa na polisi wa Kenya kwa kukosa nyaraka za utambulisho kufuatia mchakato wa kuhakiki wakiwa jela huko Nairobi tarehe 9 April, 2014. [Tony Karumba/AFP]
    Wanaume walioshikiliwa na polisi wa Kenya kwa kukosa nyaraka za utambulisho kufuatia mchakato wa kuhakiki wakiwa jela huko Nairobi tarehe 9 April, 2014. [Tony Karumba/AFP]
Wakati ofisi ya utoaji leseni za silaha huko Nairobi ilipofungwa Mei 2013, Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo alisema ilikuwa ni hatua ya muda kuwezesha serikali kufanya mageuzi na kuangalia upya historia za wamiliki silaha wenye leseni sasa.
Waombaji wa leseni za kumiliki silaha kwa sasa wanataka ruhusa ya kuzuia kwa muda kuondolea, wakisema kuendelea kwake kunawapa adhabu kwa makosa ya maofisa watoa leseni ambao wanapaswa kuwajibishwa kwa matendo yao.
Lakini Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Taifa Joseph Ole Lenku alisema serikali haitasalimu amrri kushinikiza kuondolewa kwa marufuku hayo hadi itakaporidhika kwamba uadilifu wa mchakato wa utaoaji leseni hauathiri.
"Kuna silaha nyingi katika mikono isiyo salama ambayo inatoa mweleko wa wasiwasi na kitisho kwa usalama wa nchi," aliiambia Sabahi.
Kuongezeka kwa idadi ya silaha zilizotolewa leseni kwenye mikono ya raia kunatoa ishara ya tahadhari, Lenku alisema, akiongezea kwamba maofisa wa serikali wanahofia silaha kuwa kwa wahalifu.
Uhakiki wa kuangalia na kulinganisha na rekodi za uhalifu kumeibua bendera nyekundu kuhusu idadi ya wamiliki wa silaha hivi sasa, alisema, na ripoti ya upelelezi inaonyesha baadhi ya silaha hizi zimetumika katika kufanya uhalifu.
"Ni wazi kwamba tumejikuta katika hali hiyo kwa sababu ya vitendo vya rushwa katika mchakato wa utoaji leseni, lakini tunasahihisha makosa hayo," Lenku alisema. "Kuondoa tatizo hilo kikamilifu, uchunguzi wa jumla kwa lengo la kurekebisha mchakato wa utoaji leseni na kuangalia upya wamiliki waliosajiliwa sasa ni muhimu."

Mchakato wa utoaji leseni uko katika uhakiki

Uhakiki unafanywa na maofisa wa Idara ya Uchunguzi wa Uhalifu (CID) ambao wataipa serikali ripoti ya kina baada ya kukamilisha kazi yao, inayotarajiwa kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, Lenku alisema.
Ripoti hiyo itabainisha wamiliki wa silaha na kuhakiki historia zao binafsi na kuangalia rekodi za matibabu,namna walivyopata leseni zao na kwa lengo lipi, na kuonyesha aina ya silaha anayomiliki, imekuwa inavyotumika na namna inavyohifadhiwa, alisema.
Katika mchakato wa utoaji leseni ya silaha uliokuwepo, muombaji alitakiwa kuwasilisha cheti halisi cha maadili mema kutoka kwa CID na nakala ya kadi zake za utambulisho kwa Ofisa mkuu wa kikosi wa Kitengo cha Polisi, ambaye baadaye huwasilisha maombi hayo kwa Kamati ya Usalama ya Wilaya ikiwa na maoni.
Kisha maombi yanapelekwa kwa kamati ya Usalama ya Jimbo, ambayo inayapitia na kutoa mapendekezo yake kwa Inspekta Jenerali wa Polisi, ambaye anatoa uamuzi wa mwisho.
Kisha Inspekta Jenerali wa Polisi hutuma maelezo ya maandishi kwa mkuu wa ofisi ya utoaji leseni