Baada ya miaka saba ya ukulima ndipo serina alipojitosa
rasmi katika biashara ya kutengeneza batiki kwa kuanzia na mtaji wa shilingi
16,000.
Alisema kuwa kabla ya kuanza kutengeneza batiki alitumwa na
kanisa la Moravian ofisi ya wilaya mkoani Rukwa, iliyo kuwa chini ya uongozi wa
mchungaji Kibona na kamati yake kwenda kusomea utengenezaji wa batiki kwenye
jingo la mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Selina aliongeza kuwa baada ya kuhitimu mafunzo ya wiki mbili
ndipo alipo ludi rasmi kanisani , na kuanza kutoa mafunzo kwa akinamama,
wakinababa, na vijana wa madhehebu mbalimbali.
Anasema alifanya kazi hiyo kuanzia mwaka 1990 mpaka 2003 na ndipo walipo hamia
mkoani tabora, baada ya mumewake kupata uhamisho wa kikazi.
Anasimulia kuwa wakati akiwa mkoani tabora aliendelea na kazi
yake ya kufundisha utengenezaji wa batiki, safari hii akiwafundisha hata
waumini wa madehebu ya kiislamu pamoja na wapagani.
Alifungua duka kubwa la batiki na nguo
aina zote kama vile suruari ,mashati, vitambaa vya suti, vitenge vya
waksi, magauni ya akina mama, watoto nk ikiwa
ni utoaji huduma kwa jamii.
Alisema mwezi aprili mwaka 2009 wakati akiwa safarini mkoani
mbeya kumuuguza mama mkwe wake , alipewa taarifa na wafanyakazi wake kwamba
majambazi wamevunja duka na kuiba kila kitu.
Alisema kuwa pamoja na kupata
taarifa hizo lakini hakufadhaika sana kwa sababu alimtegemea sana mwenyezi
mungu , kwamba atamrudishia zaidi ya vile vyote vilivyopotea.
Mwaka 2010 selina alijifunza utengenezaji wa sabuni za kuogea
na kufulia za miche na za maji.
Alimtaja mwalimu wake kwa jina la elbariki mchau kuwa ndiye
aliyemfundisha kutengeneza sabuni za aina mbalimbali , pamoja na somo la
biashara la kujua faida na hasara.
Pia alimfundisha kutumia vitabu vya aina mbalimbali vya
kupokelea na kutoa , na kumwelekeza
jinsi ya kusajili biashara.
Alisema kuwa anamshukuru sana mwalimu wake kwa kumtoa katika janga la usingizi ,na
kumfikisha hapa alipofikia leo.
Alisema alipo rudi nyumbani Mbeya mwaka 2011 alisikia tangazo
redioni likiwahitaji wajasiliamali waende Sido wakachukue mafunzo ya kuendesha
biashara zao kwa kutafuta masoko, kutunza kumbukumbu na kuendesha biashara kwa
faida.
Kwa vile wajasiliamali wengi walijitokeza kwenye mafunzo
hayo, ilibidi ufanye mchujo mkubwa ilikupata idadi ya watu wanaofikia 35.
Mafunzo yaliyokuwa yakitolewa yalikuwa ni ya miezi minne
hivyo mchujo uliendelea kutolewa, kwa njia ya kufanya mitihani ambapo walio
shindwa walikuwa wanaondolewa.
Selina alisema kuwa walewaliokuwa wanashinda kwenye hiyo
mitihani ya kila mwenzi walikuwa wanapewa shilingi milioni 1.1 ya Ruzuku
kwaajili ya kuinua biashara zao.
Akifafanua zaidi selina alisema kuwa yeye alipewa ruzuku ya
shilingi milioni 4.4 kwa vile alikuwa miongoni mwa washindi wa miezi minne mfululizo.
Mpaka kufikia sasa mjasiliamali huyo anamiliki duka kubwa la
sabuni za aina zote paoja na batiki lililopo katika maeneo ya uwanja wa
maonyesho ya nanenane, mkabara na kituo cha polisi wa usalama barabarani na
huku akiendelea na shuguli ya kuwafundisha wajasiliamali.
Selina amesema kuwa pamoja na kupitia matatizo mbalimbali
kamavile kuibiwa kwenye duka lake na kumfilisi kabisa lakini malengo yake ya
baadaye,ni kwamba iwapo atapata wafadhili anategemea kufungua shule yake ya
ujasiliamali.
Mafunzo atakayo yatoa katika shule yake ni kama vile
utengenezaji wa sabuni za miche, za kuogea, za maji aina zote, za chooni
Multipurpose Detergent, Shower Jelly, shampoo, mishumaa, sabuni ya Ubuyu, Uyoga
na Unga wa lishe.
Pia alizitaja batiki za aina zote na vikoi na ushonaji wa
foronya, mashuka (kudalizi) pamoja na nguo aina mbalimbali, vipochi na vikapu.
Alisema pia kuwa watafundisha usindikaji wa vyakula
mbalimbali mfano unga wa lishe, unga wa ubuyu, kusindika majani ya ubuyu,
mafuta ya ubuyu, kusindika mboga mbalimbali za majani, Chilly Sauce, tomato
Sauce, Mango Peacow Clips, Bisi na utengenezaji wa Keki za aina zote.
Mjasiliamali huyo pia alizitaja rangi za nyumba za maji na
mafuta, na mwisho akasema atatoa mafunzo ya salon, na jinsi ya kuendesha
biashara hiyo kwa faida.
Ametoa wito kwa wananchi kuto kukaa bule bila kufanya kazi
hasahasa wakina mama, na badala yake wajishughulishe ili kuinua vipato vya
familia zao na taifa kwa ujumla.
Na mwisho amewataka pia wazazi kuwaleta vijana wao pamoja na
watu wazima kwenda kujifunza katika kampuni ya kiwanda cha sabuni cha mount
Mbeya, ili wapate ujuzi kwa kujiendeshea maisha yao wenyewe.
Anapatikana kwa :0755 351381