Waalimu i hadi wawili katika shule za Njombe

Salama Lupenza wa CWT wilaya ya  NjombeIMEBAINIKA kuwa waalimu wa sayansi katika shule za kata ni wastani wa walimu wawili na mmoja shule nzima kitu kinacho katisha tamaa kufundisha masomo hayo na kusababisha wengine kukata tamaa licha ya kila shule kuwa na maabara.

Akizungumza na kituo hiki katibu wa chama cha waalimu Tanzania wilaya ya Njombe, Salama Luprnza (Pichani) amesema kuwa kwa shule za wilaya yake zina wastani wa waalimu 2 na mmoja anaye fundisha kidato cha kwanza mpaka cha nne.
Lupenza amesema kuwa licha ya kuwepo kwa maabara katika kila shule za wilaya hiyo lakini waalimu ni tatizo na kuwa baadhi ya maabara hizo hazina vifaa vilivyo kamilika na kusababisha wanafuzi wengi kukimbia masomo hayo.

Hata hivyo Lupenza amesema kuwa anaona kuna mahari taifa lilikosea kwa kutoi toa hamasa kwa wanafunzi kupenda masomo hayo kusababisha kuwa wanafunzi wachache ambao wanaingia wanagawanyika wengine wakienda kusomea Udaktari Uinginia na wengine kuingia katika fani ya Ualimu.   


Lupenza anatoa wito kwa wanafunzi kuyapenda masomo ya sayansi ili kulikomboa taifa na kuwa kwa sasa chama kina mpango wa kuhakikisha kuwa serikali kutoa motisha kwa waalimu hao na kuwa hapo baadae waalimu hao huenda wakawa na mishara ya tofauti na waalimu wengine