WAWEZESHAJI wa Mradi wa kunusuru kaya masikini
unaoendeshwa na mfuko wa maendeleo ya jamii (TASSAF) awamu ya tatu wametakiwa
kutowapendelea ndugu zao katika utekelezaji mradi huo kwa jamii.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya wa
Njombe Sarah Dumba wakati akifungua mkutano wa
kuwajengea uelewa wawezeshaji wa mradi huo kwa lengo la kuhakikisha
unawanufaisha walengwa ambao ni familia zenye hali duni ya maisha
na watoto ikiwa ni utatuzi wa changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji
wa TASSAF awamu mbili za awali.
Dumba alisema kuwa ni jambo la kushuguru mfuko huo kwa
kuichagua wilaya yake kutekelewa kwa mradi huo kwa kunusuru familia zinazo ishi
katika maiya ya hali ya chini.
Aidha Dumba alisema kuwa wawezeshaji hao wajitahidi
kuhakikisha wanawezesha walengwa wa mradi huu na kuhakikisha malengo ya mradi
yanaonekana kwa matunda bora.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Tassaf Taifa Peter
Luanda alisema mradi huo umelenga kuzifikia kaya milioni
moja (Mil 1) ambazo zinaishi katika mazingira magumu na kwa awamu ya kwanza
utachukua maeneo machache kwa sababu bado wanafanya tathmini na baada ya
kumalizika wataongeza vijiji vingine.
Luanda alisema kuwa mradi huo umelenga kuboresha maisha,
kutoa ajira kwa wenye uwezo wa kufanya kazi, kuboresha miundombinu ya maji,
afya na elimu, kutoa ruzuku kwa familia maskini hasa akina mama wajawazito
pamoja na watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano.
Mradi huo uliozinduliwa Agosti 2012 Mkoani Dodoma
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Jakaya Kikwete, Utekelezaji wa
mradi ukianza mwezi Februari 2013 na lengo lake ni kutambua kaya masikini na
umeanza na Halmashauri 16 Nchini na inatarajia kuzifikia zote 161