MKUU wa Mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi amekemea vikali tabia ya baadhi ya wanaume kuwaharibia masomo wanafunzi wakike kwa kuwarubuni kimapenzi na hivyo kuwaagiza wakuu wa wilaya na watendaji Mkoani humo kuwakamata na kuwafungulia kesi za ubakaji wale wote watakaohusika kwenye tabia hizo mbovu.
Kauli hiyo imetolewa na Dr. Nchimbi mwishoni mwa wiki katika maafari ya kwanza ya kidato cha nne shule ya sekondari ya wasichana ya Anne Makinda iliyoko Ihanga Mkoani Njombe, na kutoa agizo kwa wamendaji na kukemea tabia hiyo.
Ameitaka jamii itambue kuwa kuelimisha mtoto wa kike ni sawa na kuelimisha Taifa kwa ujumla pia aliwataka wanafunzi shuleni hapo kutambua kuwa bado wanasafari ndefu ya elimu kwani ulimwengu wa leo ni wa kisomi na elimu ya msingi ni shahada ya kwanza.
Aidha amesisitiza shule kutengewa Ardhi za kutosha ili kuruhusu upanuzi na maboresho ya miundombinu na matumizi mengineyo kama kuanzisha kidato cha tano na sita na pia miradi ya shule ya uzalishaji.
Mkuu wa shule hiyo Veronica Mlozi amesifia kiwango cha taaluma shuleni hapo kwani kwa miaka miwili iliyopita shule imefanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya kidato cha pili, Mwaka 2012 waliofanya mtihani 82 na walifaulu wote na kushika nafasi ya nne kimkoa. Mwaka 2013 waliofanya mtihani walikua 91 na kufaulu 90 na kushika nafasi ya 6 kimkoa kwa wastani wa jumla 66.2 (B).
Vilevile katika ngazi ya taifa, shule ilifanikiwa kushika nafasi ya 1 kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo kati ya shule za kata.
Changamoto inayo ibabili shule hipo ni uhaba walimu wa sayansi, ukosefu wa nishati ya uhakika ya umeme, kutokuwa na zahanati shuleni hapo, hitaji la gari la shule kwa ajili ya usafiri. Vilevile Eneo la Ardhi ya shule ni finyu na tayari malengo ya shule ni kuanzisha kidato cha tano na sita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)