MKUU wa Njombe Dkt.
Rehema Nchimbi amesema kuwa watakuwa mkali kwa viongozi wa siasa watakao
wadanganya wananchi na kuwa ujenzi wa maabara ndio unakao waongezea kura
viongozi wa siasa kama watakamilisha mapema.
Wito huo umetolewa wakati wa hafla fupi ya kukaribishwa
mkoani Njombe, Alisema kuwa kwa chama chochote kitakacho wadanganya wananchi
atakuwa mkali na hatakubaliana,na kuwataka viongozi hao wajitahidi
kuwaunganisha wananchi na sio kuwadanganya.
“Sitakubari kuona viongozi wa siasa kutoka chama chochote
kitakacho wadanganya wananchi eti serikali haijafanya chochote huo ni uongo na nitapambana nao,” alisema Dkt.
Nchimbi.
Alisema kuwa kwa suala la ujenzi wa maabara wananchi
wasidanganywe kuwa zisubiri uchaguzi vitu vyote vitasimama lakini si ujenzi huo
ni razima ukamilike katika shule kila shule katika mkoa huu.
Alisema kuwa ujenzi huo utalipatia taifa wataalamu wa Sayansi
na kuwa viongozi wa siasa wasidanganywe kuwa ujenzi wa baabara utampunguzia kura
na kuwa mtu atakaye sema kuwa maabara zitawanyima kura huyo ndio mchawi wa kura
za viongozi watakao gombea tena.
“Mtu atakaye jitokeza kupinga maabara na kukuambia kiongozi
kuwa ujenzi huo utakunyima kura basi huyo ndio mchawi wa kura zako maabara ndio
chanzo cha kura zako ukikamilisha ujenzi wa maabara utaweza kupata ushindi wa
kishindo, kwa sababu maabara ni razima ni kwamaslahi ya watoto wetu ili wafanye
vizuri katika masomo ya sayansi ” aliongeza Dkt. Nchimbi.
Alisema kuwa hatopenda kusikia kero yoyote ya kusumbuliwa
kwa wananchi na kuwa watendaji na viongozi wa siasa wanapo tekeleza mirandi
mbalimbali wasiwape kero wananchi na kuwa wawaelimishe wananchi miradi hiyo
kabla ya kuanza kutekeleza.
Dkt. Nchimbi aliongeza kuwa anatoa onyo kwa watendaji wanao
pitisha misako ya kodi na kusababisha kero kwa wananchi kwa kisa cha kutekeleza
majukumu ya kazi kwani wenginge wanachukua fulsa hiyo kuihujumu serikali.
Aidha Dkt Nchimbi aliongeza kuwa elimu ya kupiga kura
inatakiwa kutolewa kwa wanachi bali kwa kuangalia ni nani anayetoa elimu bila
kutaja chama wala kufanya kampeni kwani mda wa kampeni bado haujafika.
Alisema kuwa wananchi waelimishe kuhusu kujiandikisha katika
dar\ftari ya kupigia kura na uchaguzi ukifika utafanywa na watanzania na kuwa
hatakama mtu sio mtanzania na anapendwa kwa kiasi gani lakini hataruhusiwa
kupiga wala kupigiwa kura.
Alisema kuwa wananchi wote wenyesifa wahamasishwe kwenda
kupiga kura wakati ukifika na kuwa vituo viwekwe wazi ili kila mwananchi
afahamu niwapi ataenda kupigia kura wakati ukifika.MKUU wa Njombe Dkt.

afahamu niwapi ataenda kupigia kura wakati ukifika.