- Mamia wamsindikiza Askofu Cliopa.
- Waongozwa na kiongozi Mkuu wa KKKT Malasusa.
- Amezikwa maeneo ya kanisa hilo Njombe kwenye viwanja vya makaburi ya viongozi.
Waombolezaji wakiwa katika mazishi
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Katikati, akiwa katika mazishi ya Askofu mstaafu
mama mjane wa marehemu
Mama mjane wa marehemu akiweka Udongo katika Nyumba ya Milele ya askofu Cliopa
Mama njane akiweka taji la maua
Mwakilishi wa Shehe wa Mkoa aliweka taji nae.
Kiongozi mkuu wa Kanina KKKT akiweka shahada la maua katika Kaburi
Mkuu wa mkoa alipana nafasi ya kutoa neno la faraja kwa wafiwa
Kiongozi wa mkuu wa KKKT Tanzania, Marasusa akizungumza na mamia ya waombilezaji
KIONGOZI Mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kiluteri (KKKT) Alex
Malasula amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali hapa nchini kuacha mara moja
kufanya uovu wa kutumia vibaya mali za Umma na kujitete.
Akihubiri katika madhishi ya Askofu Mstaafu wa kanisha hilo
jimbo la Njombe, Askofu Cliopa Lukilo, jana aliye fariki Novemba 13, aliwaambia
waombolezaji kuw aviongozi wa sasa wamekuwa wakifanya uovu na kujikinga kwa
kujitetea kwa wepesi.
Alisema kuwa viongozi wa miaka ya sasa wamekuwa wakifanya
maovu ya kutumia vibaya pesa za umma na kuwa wepesi wa kujitetea kwa
kucheleweza kudaiwa wakati wakitafuta namna ya kukepa tuhuma.
Alisema kuwa kufanya hivyo si vizuri na kuwasii viongozi
kufanya kazi bila kuharibu mali za wananchi kwa kuzitumia vizuri.
Alisema kuwa viongozi wengi hawapendi kutubu na wamekuwa
mafundi wa kujitetea kwa kusingizia katiba na kuwa wanasema jambi lipo
mahakamani halijadiliki.
“Watu wengi sasa hivi ukiwaambia kutubu hawakuelewe
wanatishia watu kuwashitaki, wansema jambo hili lipo mahakamani halijadiliki,
mara umenichafua, dawa ya zambi ni kutubu na sio kujitetea,” alisema Malasula Sikiliza sauti hapa......
Alisema ukiona kitu kinacheleweshwa cheleweshwa ujue
kinatafutiuwa namna ya kujitetea.
Malasusa alisema kuwa Marehemu alikuwa akipigania haki za
watoto wakike kwa kufungua shule ili kuwaondoa katika kazi za ndani.
Alisema kuwa ni vyema wanadam wakatambua wakati wowote
wanaweza kuitwa kwani marehemu aliwahi kuugua lakini sasa amefariki kuugua
bila.
Alisema kuwa marehemu alifariki siku nne baadae baada ya
kusema kuwa yeye amejiandaa kufa wakati akifungua mkutano wa umoja wa wanawake
wa makanisa mkoani Njombe.
Alisema kuwa marehemu alitaja mara nne kuwa anejiandaa kuwa
akisema “Mimi nimejiandaa kufa, mini nimejiandaa kufa vizuru” alisema wakati wa
kufungua mkutano huo na kufa siku nne baadae.
Aidha kanisani hapo zilizomwa salamu za rambilambi kutoka
katika viongozi mbalimbali kutika hapa nchini na nje ya nchi huku kwa hapa
nchini Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa salamu zake zilisomwa kanisani hapo.
Viongozi wa serikali katika mazishi hayo alihuzuria mkuu wa
Mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi, ambapo aliomba viongozi wa dini kuwaombea
viongozi wa Umma ili kuepuka na maovu.
Dr. Nchimbi alisema kuwa viongozi waombewe ili wasiweze
kutafuna mali za umma na kuwa watiifu wanavyo ongoza wananchi mpaka wanamaliza
mda wao wa kuongoza kwani viongozi hao ni moja ya kondoo wanao wachunga.